Thursday, June 19, 2025

KATIBU MKUU MKOMI ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA NA TAASISI ZA UMMA KWENYE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, ATOA SHUKRANI KWA USHIRIKI

 Na. Mwandishi Mwetu-Dodoma

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametembelea mabanda ya Wizara na Taasisi za Umma ili kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na ofisi hizo pamoja na kutoa shukrani kwa ushiriki mkubwa katika Maadhimisho hayo ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025.

“Ninapongeza na kutoa shukrani nyingi kwa Wizara na Taasisi zote za Umma zilizoshiriki katika Maadhimisho haya ya Wiki ya Utumishi wa Umma, zimeonesha ushirikiano mkubwa na idadi ya ushiriki imekuwa kubwa,” amesema Bw. Mkomi

Bw. Mkomi ameseongeza kuwa, kupitia maadhimisho hayo wananchi wanapata fursa ya kuhudumiwa moja kwa moja, kufahamu majukumu ya Wizara na Taasisi pamoja na kupata mrejesho wa utendajikazi kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma.

Aidha, Katibu Mkuu Mkomi ameendelea kutoa wito kwa Watumishi wa Umma, Wananchi na Wadau mbalimbali kuendelea kutembelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma ili kupata huduma mbalimbali.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kulia) akimshukuru Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi (kushoto) kwa kutembelea mabanda mbalimbali kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma. 


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akizungumza na Maafisa wa Wizara ya Katiba na Sheria wakati alipotembelea katika banda la ofisi hiyo kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la TAKUKURU kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko (TPSC), Bw. Shakiru Abdulkarim alipotembelea banda la Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kulia) akipokea nyaraka mbalimbali zinazoelezea elimu juu ya haki na wajibu wa watumiaji wa huduma za usafiri wa anga kutoka kwa Maafisa wa TCAA alipotembelea banda la ofisi hiyo kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ofisi yake wakati alipotembelea banda la ofisi hiyo kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Mwonekano wa baadhi ya mabanda mbalimbali ya Wizara na Taasisi za Umma yaliyopo Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma yanayotoa huduma katika Wiki ya Utumishi wa Umma.


Mwonekano wa baadhi ya mabanda mbalimbali ya Wizara na Taasisi za Umma yaliyopo Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma yanayotoa huduma katika Wiki ya Utumishi wa Umma.


 

No comments:

Post a Comment