Na. Veronica Mwafisi na Eric Amani-Dodoma
Tarehe 05 Juni, 2025
Viongozi katika Utumishi wa Umma wametakiwa kutumia kikamilifu fursa ya mafunzo wanayoyapata kutoka Serikalini na kwa wadau mbalimbali ili kuimarisha utendaji kazi kwa ustawi wa taifa.
Hayo yamesemwa leo na Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, SACP. Ibrahim Mahumi wakati akifunga mafunzo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa, Wizara na Taasisi za Umma yaliyolenga kuwajenga kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za Serikali.
Amesema Serikali imekuwa ikitoa mafunzo kwa viongozi kutokana na dhamira ya dhati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samila Suluhu Hassan ya kuhakikisha viongozi kwenye Utumishi wa Umma wanakuwa na uelewa mpana utakaowasaidia kutekeleza majukumu ya serikali kikamilifu.
SACP. Mahumi amesema, mafunzo hayo yamejumuisha kundi la kuanzia mwezi Agosti 2021 hadi 2024 lenye viongozi 62 kutoka Wizara 11, Taasisi za Umma 8 na Sekretarieti za Mikoa 16.
Ameongeza kuwa, makundi mengine ya viongozi ambayo hayajafikiwa katika mafunzo hayo, watapatiwa kulingana na mipango iliyowekwa na serikali katika kuhakikisha kila kiongozi kwenye utumishi wa umma anapata mafunzo elekezi kwa lengo la kuboresha utendajikazi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika amesema Idara anayoiongoza imekuwa ikitoa mafunzo kwa Viongozi na watumishi wa umma ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha.
Bi. Mavika amesema viongozi hao wamepata nafasi ya kujifunza masuala ya maadili, kupata uzoefu kutoka kwa baadhi ya viongozi wastaafu, utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka, itifaki na ustaarabu pamoja na utamaduni wa kitaasisi.
Aidha, Mkurugenzi Mavika amesema mafunzo ni suala endelevu, hivyo viongozi na watumishi wanapaswa kuendelezwa kwa kujengewa uwezo katika maeneo mbalimbali ya kazi ili wafahamu namna ya kutekeleza majukumu yao.
Naye, Mkurugenzi Idara za Tawala za Mikoa-TAMISEMI, Bi. Beatrice Kimoleta ameipongeza Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa kuandaa mafunzo hayo kwa viongozi wa Mikoa na Halmashauri ambayo yatawasaidia kushughulikia masuala mbali mbali yanayowahusu watumishi wa umma na wananchi.
Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kupitia Idara ya
Uendelezaji Rasilimaliwatu imehitimisha mafunzo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi
na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa, Wizara na Taasisi za
Umma yaliyofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Jiji Dodoma.
Mwakilishi wa
Katibu Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP.
Ibrahim Mahumi akizungumza na Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka
Sekretarieti za Mikoa na Wizara wakati akifunga mafunzo yaliyolenga kuwajengea
uwezo Viongozi hao kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa
shughuli za kiutumishi yaliyofanyika Mtumba katika ukumbi wa Jiji Dodoma.
Sehemu
ya Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa
na Wizara wakiwa katika mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Uendelezaji
Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa lengo la kuwajengea uwezo Viongozi
hao kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za
kiutumishi yaliyofanyika Mtumba katika ukumbi wa Jiji Dodoma.
Mkurugenzi
Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bi. Leila Mavika akitoa maelezo ya awali
kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP.
Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) kufunga mafunzo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka
Sekretarieti za Mikoa yaliyolenga kuwajengea
uwezo Viongozi hao kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa
shughuli za kiutumishi.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI,
SACP. Ibrahim Mahumi (katikati mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya
pamoja na Makatibu
Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa na
Wizara mara
baada ya kufunga mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi hao kifikra,
kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiutumishi yaliyofanyika
Mtumba katika ukumbi wa Jiji Dodoma.
Mshauri
Elekezi, ambaye ni Mkufunzi, Bw.
Moses Samora akiwasilisha mada
kuhusu namna ya kuwa kiongozi mwenye maono, thamani na mbinu za kulea watumishi wanaowaongoza wakati
mafunzo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka
Sekretarieti za Mikoa na Wizara yaliyoandaliwa na Idara ya Uendelezaji
Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi
hao kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za
kiutumishi.
Sehemu ya Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mafunzo kwa
Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi
kutoka Sekretarieti za Mikoa na Wizara yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi
hao kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za
kiutumishi.
Mkurugenzi
Idara za Tawala za Mikoa-TAMISEMI, Bi. Beatrice Kimoleta akitoa pongezi kwa
Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa kufanya mafunzo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka
Sekretarieti za Mikoa na Wizara
yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi hao kifikra, kitabia na mtazamo
kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiutumishi.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi (katikati
mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu
Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa na
Wizara mara baada ya kufunga mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi
hao kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za
kiutumishi yaliyofanyika Mtumba katika ukumbi wa Jiji Dodoma.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi (katikati
mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti iliyoandaa
mafunzo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka
Sekretarieti za Mikoa na Wizara yaliyofanyika Mtumba katika ukumbi wa Jiji
Dodoma.
Sehemu
ya Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa
na Wizara wakiwa kwenye mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi hao
kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiutumishi
yaliyofanyika Mtumba katika ukumbi wa Jiji Dodoma.
No comments:
Post a Comment