Na Lusungu Helela - TABORA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema
anatamani kuona Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) inakuwa
kimbilio la Walimu ambao ni kundi kubwa katika Utumishi wa Umma kwa kutenda haki pindi
inaposhughulikia mashauri ya nidhamu na rufaa za Walimu
Amesema haifurahishi kuona Walimu
wanapoteza ajira kwa ukiukaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu katika Utumishi wa Umma
ilhali TSC ipo.
Mhe. Simbachawene ametoa kauli
hiyo leo wakati akifunga mafunzo
ya Uendeshaji wa Mashauri ya Nidhamu na Rufaa kwa Walimu yaliyofanyika kwa
muda wa siku tatu katika Chuo Cha
Utumishi wa Umma, Tanzania, Kampasi ya Tabora yaliyoendeshwa na TSC.
Amesema TSC ndiyo mlezi wa Walimu,
hivyo Wajumbe na watumishi wa Tume hiyo watoe elimu kwa Walimu katika masuala
muhimu yanayohusu utumishi wao kwa kuzingatia jukumu lake la ulezi, adhabu ya
kufukuzwa kazi iwe ni hatua ya mwisho pale inapotokea Mwalimu kutotii
yale anayoelekezwa.
Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Simbachawene
amewataka Maafisa Elimu walioteuliwa kuwa Wajumbe wa Kamati za Ajira,
Upandishaji Vyeo na Nidhamu wa Tume ya Utumishi wa Walimu ngazi ya
Wilaya wakatumie mafunzo hayo waliyoyapata kama nyenzo ya
kuboresha utendaji kazi kwa kutoa haki kwa Walimu wenye mashauri ya nidhamu na
rufaa.
" Ni matumaini yangu
kuwa baada ya mafunzo haya hatutasikia au kuona uamuzi wa shauri unakatiwa
rufaa Tume ya Utumishi wa Walimu Makao Makuu kwa kuamuriwa bila
kuzingatia matakwa ya Sheria, Kanuni na Taratibu zinazowaongoza katika
kufikia uamuzi kwa haki na usawa" amesema Mhe.Simbachawene.
Vile vile Mhe. Simbachawene
ametoa rai kwa Wajumbe hao kuhakikisha wanazingatia Sheria, Kanuni na
Taratibu zinazosimamia uendeshaji wa mashauri ya nidhamu pindi
wamaposhughulikia mashauri ya nidhamu na rufaa.
Awali, Mwenyekiti wa Tume ya
Utumishi wa Walimu Prof. Masoudi Muruke amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha kunakuwa na Walimu ambao wanajituma na
wanaozingatia maadili ya kazi yao kwa ajili ya kuwalea watoto kwa usahihi na
hivyo kuboresha elimu nchini kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Ummana Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akizungumza wakati akifunga mafunzo ya Uendeshaji wa Mashauri ya Nidhamu na Rufaa kwa Walimu yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu katika Chuo Cha Utumishi wa Umma, Tanzania, Kampasi ya Tabora yaliyoendeshwa na TSC.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Walimu (TSC) Prof. Masoudi Muruke alipowasili kwa ajili ya kufunga mafunzo ya Uendeshaji wa Mashauri ya Nidhamu na Rufaa kwa Walimu yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu katika Chuo Cha Utumishi wa Umma, Tanzania, Kampasi ya Tabora yaliyoendeshwa na TSC.
Baadhi ya Maafisa Elimu walioteuliwa kuwa Wajumbe wa Kamati za Ajira, Upandishaji Vyeo na Nidhamu wa Tume ya Utumishi wa Walimu ngazi ya Wilaya wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Ummana Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene wakati akifunga mafunzo ya Uendeshaji wa Mashauri ya Nidhamu na Rufaa kwa Walimu yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu katika Chuo Cha Utumishi wa Umma, Tanzania, Kampasi ya Tabora yaliyoendeshwa na TSC.
Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Ernest Mabonesho akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene wakati akifunga mafunzo ya Uendeshaji wa Mashauri ya Nidhamu na Rufaa kwa Walimu yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu katika Chuo Cha Utumishi wa Umma, Tanzania, Kampasi ya Tabora yaliyoendeshwa na TSC.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Cornel Magembe ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene wakati akifunga mafunzo ya Uendeshaji wa Mashauri ya Nidhamu na Rufaa kwa Walimu yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu katika Chuo Cha Utumishi wa Umma, Tanzania, Kampasi ya Tabora yaliyoendeshwa na TSC.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Walimu (TSC) Prof. Masoudi Muruke akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene wakati akifunga mafunzo ya Uendeshaji wa Mashauri ya Nidhamu na Rufaa kwa Walimu yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu katika Chuo Cha Utumishi wa Umma, Tanzania, Kampasi ya Tabora yaliyoendeshwa na TSC.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Ummana Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwakabidhi vyeti Maafisa Elimu walioteuliwa kuwa Wajumbe wa Kamati za Ajira, Upandishaji Vyeo na Nidhamu wa Tume ya Utumishi wa Walimu ngazi ya Wilaya wakati akifunga mafunzo ya Uendeshaji wa Mashauri ya Nidhamu na Rufaa kwa Walimu yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu katika Chuo Cha Utumishi wa Umma, Tanzania, Kampasi ya Tabora yaliyoendeshwa na TSC.
No comments:
Post a Comment