Na Mwandishi Wetu – DODOMA
“Serikali imeongeza bajeti, kutoa vibali vya
ajira na kuruhusu ununuzi wa vifaa muhimu kwa taasisi husika ili kuongeza
ufanisi wa mapambano haya,” amesema Mhe. Simbachawene.
Aidha, ameeleza kuwa elimu kuhusu madhara ya
rushwa imekuwa ikitolewa kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu, ili kujenga
jamii yenye uelewa na inayochukia rushwa.
“Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika
mapambano dhidi ya rushwa kila mwaka. Haya ni mafanikio makubwa yanayotokana na
jitihada za pamoja za wananchi wote,” ameongeza.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin
Chalamila, amesema rushwa ni kikwazo kikubwa kwa ustawi wa wananchi, kwani
inadhalilisha utu wa jamii.
“Kuondoa vitendo vya rushwa kutasaidia kujenga
jamii yenye usawa, kuheshimiana na inayowajibika,” amesema Chalamila.
Amesisitiza kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua haki ya kila raia kupata huduma bila upendeleo, hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kushiriki katika vita dhidi ya rushwa.
Bw. Chalamila ameongeza kuwa TAKUKURU inaendelea
kubuni mbinu mpya za kushughulikia rushwa ili kuhakikisha huduma zote za
kijamii zinatolewa kwa haki bila vitendo vya rushwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA), Bw. Ali Abdalla Ali, amesema maadhimisho ya
kupambana na rushwa yana umuhimu mkubwa kwani hutoa fursa ya kutathmini hali
halisi na kupanga mikakati mipya ya kuongeza kasi ya mapambano hayo.
“Jamii sasa inatambua kuwa rushwa ni adui wa
haki, maendeleo na kwamba inachochea umaskini. Maadhimisho haya huchangia
kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wananchi na kuimarisha ushirikiano kati ya
taasisi na wananchi,” amesema.
Amesisitiza kuwa endapo kila mmoja atashiriki
kikamilifu katika vita dhidi ya rushwa, Tanzania itakuwa nchi salama, yenye
maendeleo na haki kwa wote.
Awali, Mwakilishi wa Bodi ya Ushauri ya Masuala
ya Rushwa ya Umoja wa Afrika (AUABC) , Bw. Benjamin Kapera, ameeleza kuwa
kuendelea kufumbiwa macho kwa vitendo vya rushwa kumesababisha madhara
mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuathiri michakato ya uchaguzi barani Afrika,
wagonjwa kushindwa kupata matibabu hospitalini, vijana wenye sifa kukosa haki
zao, na kudhoofisha mifumo ya utoaji haki na kusisitiza umuhimu wa kuchunguza
kwa kina madhara yanayotokana na vitendo vya rushwa.
Kwa mujibu wa Mfuko wa Mo Ibrahim, Afrika
inapoteza takribani dola bilioni 128 za Kimarekani kila mwaka kutokana na vitendo
vya rushwa, sawa na asilimia 50 ya mapato yake ya kodi na asilimia 25 ya pato
la Taifa. Kufuatia hali hiyo, Kapera amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Afrika
kuchukua hatua za haraka kushughulikia tatizo la rushwa.
Pia, ametoa wito kwa Serikali za Afrika kuwekeza
katika matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ili kuhakikisha
uwajibikaji na utoaji wa huduma kwa usawa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza leo Juni 11,2025 jijini Dodoma ,wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi,akitoa mada wakati wa Kongamano
la Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa
na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi
ya Rushwa.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bw. Crispin Chalamila akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kufungua Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Mwakilishi wa Bodi ya
Ushauri ya Masuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika,Benjamin Kapera,akizungumza
kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kufungua Kongamano la Maadhimisho ya
Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya
kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa uchumi Zanzibar (ZAECA) Bw.Ali Abdalla
Ali akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
kufungua Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani
Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu
katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Sehemu ya Wanafunzi wakifuatilia mada mbalimbali katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya
mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na
kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.




.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)



.jpeg)


.jpeg)

No comments:
Post a Comment