Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ametembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na kutoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha rasilimali fedha za ujenzi wa jengo hilo na maelekezo ambayo amekuwa akiyatoa mara kwa mara ya kuboresha shughuli za taasisi hiyo ikiwemo mchakato mzima wa ajira nchini.
Akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma leo mara baada ya kufika katika Ofisi hiyo iliyopo eneo la Tambukaleri jijini Dodoma, Mhe. Simbachawene amesema mahitaji ni mengi lakini Rais aliona ni muhimu pamoja na mambo mengine suala la ajira likapewa kipaumbele hasa kwa kuwa na jengo lake katika uendeshaji wa mchakato wa ajira.
“Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita hasa Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo mbalimbali na utashi wake binafsi wa kutuwezesha kuwa na jengo hili na majengo mengine yaliyo chini ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, haya yote yasingewezekana kwa sababu mahitaji ni mengi” Mhe. Simbachawene ameongeza.
Mhe. Simbachawene ameipongeza Bodi na Menejimenti ya Ofisi hiyo kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa jengo hilo na wote waliohusika ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuhakikisha jengo la ofisi hiyo linakamilika kwa ustadi.
“Lengo langu leo ni kuangalia jengo, kwa kweli jengo limejengwa kwa ustadi mkubwa sana, niwapongeze wataalam wote waliohusika katika ujenzi na waliosimamia, jengo lina mvuto na thamani ya fedha inaonekana.” Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Aidha, Mhe. Simbachawene amezungumzia suala la mchakato wa ajira kufanyika mikoani na kuchukua barua za ajira mikoani kuwa ni maelekezo ya Rais ambayo alielekezwa ili kupunguza gharama na muda wa wasailiwa.
“Maelekezo yote ya kuboresha mchakato wa ajira ambayo nilikuwa nikiyatoa kwa Bodi na Menejimenti nilikuwa nikipewa na Rais, hivyo hatuna budi kumshukuru kwa maelekezo yake yenye kujenga” Ameongeza.
Mhe. Simbachawene amewasisitiza watumishi wa Ofisi hiyo kuendelea kusimamia kikamilifu zoezi la usaili wa ajira na kuwa makini ili wenye sifa wapate ajira kwa haki bila upendeleo.
Naye Naibu Waziri Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ameipongeza
Sekretarieti ya Ajira kwa kuwa wepesi kupokea maelekezo mbalimbali yaliyokuwa
yakitolewa na viongozi ili kuboresha utendaji kazi wa taasisi hiyo.
Amewataka watumishi wa ofisi
hiyo kutumia ofisi hiyo mpya kama chagizo la morali ya kufanya kazi.
“pongezi kwa ofisi kuwa na
jengo lake na Mhe. Simbachawene kwa maelekezo, usimamizi na uongozi vimeonekana
kwa vitendo. Mimi ni shahidi, nimekuwa nikipokea maelezo yako ya kushughulikia
changamoto za taasisi hii.” Mhe.
Sangu amesema
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bibi Sofia Kaduma amemshuru Waziri Simbachawene kwa miongozo na maelekezo ambayo amekuwa akiyatoa kwa Bodi na Menejimenti hiyo ambayo yameongeza ufanisi na kuleta tija kwa taifa.
Kwa upande wake Katibu wa
Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, Bwana Mick Kiliba amesema
utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi hiyo ulianza tarehe mwezi
Aprili, 2022 kupitia Mshauri Elekezi wa Mradi (Chuo Kikuu cha Ardhi) kupitia
Kampuni ya ARU Built Environment
Consulting Company Limited (ABECC).
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. George Simbachawene akizungumza
na Viongozi na Watumishi ya
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) jijini
Dodoma wakati alipotembelea jengo jipya la ofisi hiyo
iliyopo eneo la Tambukareli jijini Dodoma.
Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao
wakati alipotembelea jengo jipya la ofisi hiyo
iliyopo eneo la Tambukareli jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene akifurahia jambo na Naibu Waziri wa ofisi hiyo Mhe. Deus Sangu mara
baada ya Waziri huyo kuwasili katika jengo jipya la ofisi ya Sekretarieti ya Ajira iliyopo eneo la Tambukareli jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene (wakwanza kushoto) akisalimiana na Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (wakwanza
kulia) wakati Waziri huyo alipotembelea jengo
jipya la ofisi ya Sekretarieti ya Ajira iliyopo eneo la Tambukareli jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akitoa maelezo ya awali kabla ya
kumkaribisha Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. George
Simbachawene (hayupo pichani)
alipotembelea jengo jipya la
ofisi ya Sekretarieti
ya Ajira iliyopo eneo la Tambukareli jijini
Dodoma.
Katibu wa Sekretarieti
ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (Aliyesimama)
akielezea utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene (wapili kutoka kushoto waliokaa) na
Viongozi wengine wakati Waziri huyo alipotembelea jengo jipya la ofisi
hiyo iliyopo eneo la Tambukareli jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akifurahia jambo na Viongozi wa ofisi yake na Watendaji wa ofisi ya Sekretarieti ya Ajira wakati wakikagua ukumbi wa kufanyia usaili
kwenye jengo jipya la ofisi hiyo iliyopo eneo la
Tambukareli jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuwasili katika jengo
jipya la ofisi hiyo lililopo eneo la Tambukareli jijini
Dodoma.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene akifurahia jambo
mara baada ya kukabidhiwa maua ya ukaribisho
wakati alipowasili katika jengo jipya la ofisi ya Sekretarieti
ya Ajira katika Utumishi wa Umma iliyopo eneo la Tambukareli jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (wakwanza kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti
wa Sekretarieti ya Ajira, Bibi Sophia Kaduma (wakwanza kulia) wakati Naibu
Waziri huyo alipowasili katika jengo jipya la
ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma iliyopo
eneo la Tambukareli jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bw.
Innocent Bomani (aliyenyanyua mkono) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene (aliyevaa miwani) wakati alipotembelea jengo jipya la ofisi hiyo
iliyopo eneo la Tambukareli jijini Dodoma. Wengine ni Viongozi wa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Watendaji wa Sekretarieti ya Ajira.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi (watatu kutoka kushoto) akifurahia jambo na
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Mick
Kiliba (aliyenyanyua mkono) wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
(hayupo pichani) alipotembelea jengo jipya la ofisi ya Sekretarieti ya Ajira
iliyopo eneo la
Tambukareli jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. George Simbachawene (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja
na Viongozi na Watendaji wa
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mara baada ya kutembelea
jengo jipya la ofisi hiyo iliyopo eneo la Tambukareli jijini Dodoma.
Mwonekano
wa Jengo jipya la Sekretarieti ya Ajira lililopo eneo la Tambukareli jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment