Sunday, July 20, 2025

WAZIRI SIMBACHAWENE AWAONYA WANAOHAMASISHA UVUNJIFU WA AMANI NCHINI

Na Lusungu Helela - Dodoma 

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene amewaonya wale wote wanaohamasisha uvunjifu wa amani nchini huku akiwasihi Wanawake wasijiingize kwenye  mtego huo kwani madhara yake ni makubwa.

 Mhe.Simbachawene ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua Kongamano la 16 la Wanawake Waombolezao Kitaifa waliokusanyika jijini Dodoma kwa ajili ya kuombea amani ya nchi ya Tanzania  hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi  Oktoba mwaka huu. 

 Amesema maendeleo yaliyopo nchini ikiwemo huduma za kijamii ni matokeo ya amani na utulivu uliopo, "Hatuwezi kubomoa ili tujenge upya, ni lazima tukumbatie majadiliano kama Taifa hatuwezi tukawa tunafikiria sawa ni lazima tutofautiane" amesisitiza Mhe.  Simbachawene.

 "Kuna watu wanasema Tanzania hii hakuna amani  wala maendeleo yaliyofanyika tangu tupate uhuru, hivyo tuandamane,  hapo ndipo tutapata haki yetu, wananchi kataeni huo ushetani"  amesema Waziri Simbachawene 

 Kufuatia hatua hiyo Mhe.Simbachawene amewataka Watanzania  kuwapuuza wale wote wenye maslahi binafsi wanaotaka kuwaona  wananchi wanachukiana wenyewe kwa wenyewe  na hatimaye kuanza  kuuana wao kwa wao  kwa chuki za kupandikizwa. 

 Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Tanzania  Fellowship of Churches, Godfrey Malasi amesema Kongamano hilo ni mahsusi kwa ajili ya  maombi maalum ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwisho wa mwaka  kwa lengo la kuliombea amani  Taifa la Tanzania na kuwahimiza Watanzania kumjua na kumtumikia Mungu.

 Sisi tunavyofurahia amani na utulivu tuliyonayo, wenzetu huko kwingine wanalia na kusaga meno, hivyo tuna wajibu wa kuzidi kumuomba Mungu atupe hekima ili tuzidi kuilinda amani yetu, amesisitiza Askofu Malasi.

 Vita sio nzuri kabisa,  sisi tumepewa uwezo wa kupigana vita vya rohoni ili kuzuia vita vinavyoonekana "  amesema 

 Aidha, Askofu Malasi amesema Kongamano hilo limekuwa likiombea maadili mema ya Taifa hususan katika kipindi hiki ambacho vijana wameathiriwa na vitendo vya ushoga, usagaji na utoaji mimba, vitendo ambavyo vinakwenda  kinyume na tamaduni zetu.

 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akizungumza leo  wakati akifungua Kongamano la 16 la Wanawake Waombolezao Kitaifa linalofanyika  jijini Dodoma kwa ajili ya kuombea amani ya nchi ya Tanzania  hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu

Askofu Mkuu wa Tanzania  Fellowship of Churches, Godfrey Malasi akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene kwa ajili ya kufungua Kongamano la 16 la Wanawake Waombolezao Kitaifa linalofanyika  jijini Dodoma kwa ajili ya kuombea amani ya nchi ya Tanzania  hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu

 

Baadhi ya Wanawake na Wanaume waliokusanyika jijini Dodoma kwenye  Kongamano la 16 la Wanawake Waombolezao Kitaifa wakiomba kabla Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene kufungua Kongamano hilo kwa ajili ya kuombea amani ya nchi ya Tanzania  hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa na baadhi ya Viongozi wa   Kongamano la 16 la Wanawake Waombolezao Kitaifa wakiwa wameshika bendera ya Tanzania  kwenye Kongamano hilo  linalofanyika  jijini Dodoma kwa ajili ya kuombea amani ya nchi ya Tanzania  hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu

 

Baadhi ya Wanawake wakiwa wameshika Bendera ya Tanzania katika  Kongamano la 16 la Wanawake Waombolezao Kitaifa linalofanyika  jijini Dodoma kwa ajili ya kuombea amani ya nchi ya Tanzania  hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene kufungua Kongamano hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wanawake kwenye  Kongamano la 16 la Wanawake Waombolezao Kitaifa linalofanyika  jijini Dodoma kwa ajili ya kuombea amani ya nchi ya Tanzania  hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu

 


 
Askofu  wa Tanzania  Fellowship of Churches, Bi. Malasi akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kwa ajili ya kufungua Kongamano la 16 la Wanawake Waombolezao Kitaifa linalofanyika  jijini Dodoma kwa ajili ya kuombea amani ya nchi ya Tanzania  hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu

 


 


 


 

 




 


 

 


 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


No comments:

Post a Comment