Na. Veronica Mwafisi-Lindi
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.
Juma Mkomi amekagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma
unaojengwa katika Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ili kuwasaidia
watumishi hao kuwa karibu na ofisi wanazofanyia kazi kwa lengo la kutekeleza
majukumu yao kikamilifu.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo leo, Katibu Mkuu Mkomi
amesema ujenzi wa makazi ya watumishi hao utawasaidia kuepeukana na changamoto
ya makazi ambayo imekuwa ikiwakabili na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa
ufanisi.
Amesema Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa ikiwajali sana watumishi wa
umma katika kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo utekelezaji wa mradi wa makazi
ya watumishi.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutekeleza kwa vitendo azma yake ya
kuujenga utumishi wa umma pamoja na kuboresha mazingira ya utendaji kazi wa
watumishi wa umma ili wawe na tija katika utoaji wa huduma kwa maendeleo ya
taifa,” Katibu Mkuu Mkomi ameongeza.
Bw. Mkomi amesema mradi wa ujenzi wa makazi hayo ya watumishi upo
katika hatua ya majaribio katika Manispaa ya Lindi, mkoa wa Lindi ambapo pia
unatekelezwa katika Mikoa ya Dodoma, Singida na Ruvuma.
Katibu Mkuu Mkomi katika ziara hiyo aliambatana na baadhi ya
Wakurugenzi wa ofisi yake ambapo kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha
Ufuatiliaji na Tathmini, Bw. Patrick Allute amesema Watumishi Housing Investments ndiyo kandarasi inayojenga makazi
katika mradi huo.
Bw. Allute ameongeza kuwa, mradi huo unafuatiliwa na kusimamiwa kikamilifu ili uweze kukamilika kwa wakati.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Bw. Juma Mkomi (wakwanza kushoto) akikagua maendeleo
ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma Kijiji cha
Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Bw. Juma Mkomi (aliyevaa miwani) akisisitiza jambo kwa Mwalimu Mkuu wa
Shule ya Msingi Kijiweni, Bw. Hassan Kalembo (wapili kutoka kulia) na Mwalimu
wa Taaluma wa Shule hiyo, Bw. Samson Bihole mara baada ya Katibu Mkuu huyo
kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma katika Kijiji cha
Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akitoka kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa
makazi ya watumishi wa umma katika Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi.
Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kijiweni, Bw. Hassan Kalembo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (watano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi kutoka katika ofisi yake na Viongozi na Watendaji wa Shule ya msingi Kijiweni mara baada ya Katibu Mkuu huyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma katika Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi.
Mwonekano wa jengo la mradi wa makazi ya watumishi wa
umma lililopo katika Kijiji cha
Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi.
No comments:
Post a Comment