Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 28 Julai, 2025
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora wamekumbushwa kutanguliza uzalendo wanapotoa huduma kwa
wananchi pamoja na kuwa na uelewa mpana wa masuala mbalimbali ya kiutumishi ili
waweze kutoa huduma bora kwa maslahi ya Taifa.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni
Naibu Katibu Mkuu, Bw. Xavier Daudi ameyasema hayo wakati
akizungumza na watumishi wa ofisi yake kwenye
eneo maalum la mafunzo kwa watumishi wa ofisi hiyo yanayofanyika Mtumba
jijini Dodoma kila Jumatatu ya mwanzo wa wiki.
“Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora ina
majukumu mengi ikiwemo utoaji wa huduma mbalimbali za kiutumishi hivyo, tutangulize
uzalendo na tuhakikishe tunafahamu majukumu yote ya ofisi hii ili tuweze kuwahudumia
Watumishi wa Umma na Wananchi kwa maslahi ya Taifa.” amesema Bw. Daudi.
Aidha, Bw. Daudi amesisitiza
watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kuwa waadilifu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni,
Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma wanapotekeleza majukumu yao.
Awali akiwasilisha mada kuhusu Maslahi ya
Taifa na Ulinzi wa Taifa, Balozi Omar Mjenga amesema, watumishi wa umma wana
wajibu wa kuwa wazalendo na nchi yao kwa kuzingatia utii usiokuwa na shaka,
kiapo cha utii pamoja na kujitoa kikamilifu kwa maslahi ya Taifa.
Aidha, Balozi Mjenga ameupongeza Uongozi wa Ofisi
ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora pamoja na watumishi wa ofisi hiyo kwa kuwa na
utayari wa kuandaa na kushiriki mafunzo kila Jumatatu ya mwanzo wa wiki ili
kujenga uelewa kwa watumishi hao kuhusiana na masuala mbalimbali ya kiutumishi.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais-UTUMISHI ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Bw. Xavier Daudi akisisitiza
jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha
utendaji kazi watumishi
wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Afisa kutoka Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Oswin Mkinga (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu masuala ya utendaji kazi ktk taasisi za umma wakati wa mafunzo ya kujengewa uwezo na kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Balozi
Omar Mjenga (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu Maslahi ya Taifa na
Ulinzi wa Taifa wakati wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na
Utawala Bora yaliyolenga kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi.




No comments:
Post a Comment