Na. James K. Mwanamyoto – Tabora
Tarehe 17 Disemba, 2020
Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania (TPSC) kimepongezwa kwa kutumia fedha za mapato yake ya ndani kiasi
cha shilingi bilioni 3.5 kujenga jengo la ghorofa mbili lililoanza kutumika
kutoa mafunzo kwa Watumishi wa Umma na Wananchi katika fani mbalimbali
zinazotolewa na chuo hicho kwenye Kampasi ya Tabora.
Pongezi hizo zimetolewa leo
Mkoani Tabora na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika mara baada ya kukagua jengo
jipya la TPSC Kampasi ya Tabora.
Mhe. Mkuchika amesema hatua
ya kutumia fedha za ndani kujenga jengo lenye ofisi na madarasa, linapaswa
kuigwa na taasisi nyingine za umma ambazo zinaitegemea Serikali kuwapatia fedha
kuboresha ofisi zao.
“Kitendo cha kutumia fedha
za ndani kwa maendeleo ya taifa ni jambo zuri ambalo Mhe. Rais amekuwa
akisisitiza mara kwa mara, hivyo, ujenzi wa jengo hili linanipa ujasiri wa
kuwaalika Viongozi wa Kitaifa kulizindua rasmi, huku kipaumbele kikiwa kwa Mhe.
Rais mwenyewe,” Mhe. Mkuchika amefafanua.
Mhe. Mkuchika ameongeza
kuwa, ushirikiano na uadilifu uliopo baina ya Viongozi na Watumishi ndio
ulifanikisha kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo, hivyo amewataka kuuendelea na
utamaduni huo kwa masilahi ya chuo na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Akitoa taarifa kuhusu ujenzi
wa jengo hilo, Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt.
Emmanuel Shindika amesema jengo hilo limekamilika na kuanza kutumika kabla ya
uzinduzi rasmi ili kuongeza ufanisi kiutendaji na kubaini mapungufu yanayoweza
kujitokeza kwa lengo la kuyadhibiti.
Mradi wa ujenzi wa jengo
hilo linalojumuisha maktaba, vyumba vya madarasa ya kompyuta, kumbi, madarasa
ya kawaida na ofisi za watumishi ulianza tarehe 5 Novemba, 2014 na kukamilika
rasmi tarehe 26 Machi, 2020.
1.
1. Mwonekano wa jengo jipya la Chuo Cha Utumishi wa Tanzania (TPSC) - Kampasi ya Tabora lililojengwa kwa fedha za mapato ya ndani.
1.Baadhi ya wanafunzi wakipata mafunzo katika moja ya darasa lililopo ndani ya jengo jipya la Chuo Cha Utumishi wa Tanzania (TPSC) -Kampasi ya Tabora lililojengwa kwa fedha za mapato ya ndani.
1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst)
Mhe. George Mkuchika akishuhudia mpangilio wa vitabu katika maktaba maalum
iliyoko kwenye jengo jipya la Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) -
Kampasi ya Tabora.
1. Baadhi ya watumishi wa Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzani-Kampasi ya Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika (hayupo pichani) alipoenda kukagua jengo
jipya la TPSC Kampasi ya Tabora.
1.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst)
Mhe. George Mkuchika akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzani-Kampasi ya Tabora alipoenda kukagua jengo jipya la
TPSC Kampasi ya Tabora.
1. Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika akiwasilisha kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika taarifa ya
mradi wa jengo jipya la TPSC-Kampasi ya Tabora alipoenda kukagua jingo hilo.
No comments:
Post a Comment