Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akifuatilia taarifa kuhusu mifumo ya kuhifadhi nyaraka
iliyokuwa ikiwasilishwa na Watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa
wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Dodoma yenye lengo la kufahamiana na
watumishi wa Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Salum Kyando akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Ndejembi katika Idara hiyo Jijini Dodoma
yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.
No comments:
Post a Comment