Tarehe 07 Agosti, 2022
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amezindua jengo la masjala ya ardhi kijiji cha Melela wilayani Mvomero, lililojengwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) na kumuelekeza Mtendaji wa Kijiji kuhakikisha linatumika ipasavyo kuwahudumia wananchi wa kijiji hicho.
“Serikali inataka ofisi hii iwe ni sehemu muhimu itakayowawezesha wananchi wa Melela kupata maendeleo, wataalam wote waitumie ofisi hii kuwahudumia wananchi pindi wanapofuata huduma, kama ambavyo Serikali imekusudia,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Ameongeza kuwa, uwepo wa ofisi hiyo umeondoa tatizo la uhaba wa ofisi, hivyo kuondoa kisingizio cha baadhi ya watumishi wa Kijiji cha Melela kutowajibika ipasavyo kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa Benki ya CRDB, Bw. Emmanuel Meela ameipongeza Serikali kupitia MKURABITA kwa kujenga ofisi ya Masjala ya Ardhi ambayo itawasaidia wananchi kurasimisha ardhi na kupata hati miliki za kimila ambazo zitawawezesha kukopa katika taasisi za kifedha kwa lengo kufanya shughuli za maendeleo.
Naye, Meneja wa Benki ya NMB Mvomero, Bw. Innocent Kato amewathibitishia wananchi wa Kijiji cha Melela kuwa Benki ya NMB inazitambua Hati za Hakimiliki za Kimila, na kuongeza kuwa mpaka hivi sasa benki hiyo imepokea dhamana ya takribani ya kiasi cha shilingi milioni 600 hadi 700 zilizowekwa na wananchi wenye uhitaji wa kuendesha shughuli za kiuchumi wilayani Mvomero.
Akizungumzia utayari wa taasisi za kifedha kutoa mikopo kupitia Hati za Hakimiliki za Kimila, Mratibu wa MKURABITA, Dkt. Seraphia Mgembe amewaasa wananchi wa Kijiji cha Melela kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kupata maendeleo kupitia mikopo ya kilimo na ujasiliamali.
Aidha, mmoja wa wananchi wa kijiji cha Melela Bw. Mohamed Seif ambaye amekabidhiwa Hati ya Hakimiliki ya Kimila na Mhe. Jenista Mhagama, amesema yeye ni mjasiriamali hivyo ataitumia hati hiyo kukopa katika benki za NMB na CRDB ambazo hazina riba kandamizi ili aweze kutumia mkopo huo kupata maendeleo.
Mhe. Jenista Mhagama amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini na shughuli za MKURABITA katika Manispaa ya Morogoro na Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akitoa hatimiliki za kimila kwa
mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Melela, Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani
Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga
kutoa hatimiliki za kimila na kuzindua jengo la masjala ya ardhi lililojengwa
na MKURABITA katika Halmashauri hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Melela, Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani
Morogoro mara baada ya kutoa hatimiliki za kimila kwa wananchi hao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kutoa hatimiliki za
kimila na kuzindua jengo la masjala ya ardhi lililojengwa na MKURABITA katika
Halmashauri hiyo.
Anayeshuhudia ni Mratibu wa MKURABITA, Dkt. Seraphia Mgembe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisoma maandishi ya uzinduzi wa jengo la masjala ya ardhi lililojengwa na MKURABITA katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani
Morogoro mara baada ya kuzindua rasmi masjala hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kutoa hatimiliki za
kimila na kuzindua jengo la masjala ya ardhi lililojengwa na MKURABITA katika
Halmashauri hiyo.
Mwonekano wa jengo la masjala ya ardhi, Kijiji cha Meela,
Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro lililozinduliwa na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kutoa hatimiliki za kimila na kuzindua jengo la masjala lililojengwa
na MKURABITA katika Halmashauri hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza
na wananchi wa Kijiji cha Melela, Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro
wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kutoa hatimiliki za kimila na kuzindua
jengo la masjala ya ardhi lililojengwa na MKURABITA katika Halmashauri hiyo.
Wananchi wa Kijiji cha Melela, Halmashauri ya Wilaya ya
Mvomero mkoani Morogoro wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo
pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara
yake ya kikazi iliyolenga kutoa hatimiliki za kimila na kuzindua jengo la
masjala ya ardhi lililojengwa na MKURABITA katika Halmashauri hiyo.
Mratibu wa MKURABITA, Dkt. Seraphia Mgembe akitoa taarifa
ya utekelezaji wa MKURABITA kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Jenista iliyolenga kutoa
hatimiliki za kimila na kuzindua jengo la masjala ya ardhi lililojengwa na
MKURABITA katika Halmashauri hiyo.
Meneja wa NMB tawi la Mvomero, Bw. Innocent Kato
akimthibitishia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuwa NMB inazitambua hatimiliki za kimila
zinazotolewa na MKURABITA wakati wa ziara ya kikazi ya
Mhe. Jenista katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero iliyolenga kutoa
hatimiliki za kimila na kuzindua jengo la masjala ya ardhi lililojengwa na
MKURABITA katika Halmashauri hiyo.
Afisa Uhusiano wa Benki ya CRDB, tawi la Mzumbe, Bw.
Emmanuel Meela akimthibitishia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuwa CRDB inazitambua
hatimiliki za kimila zinazotolewa na MKURABITA wakati wa
ziara ya kikazi ya Mhe. Jenista katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero
iliyolenga kutoa hatimiliki za kimila na kuzindua jengo la masjala ya ardhi
lililojengwa na MKURABITA katika Halmashauri hiyo.
Mwananchi wa Kijiji cha Melela, Halmashauri ya Wilaya ya
Mvomero mkoani Morogoro, Bw. Mohamed Seif akielezea namna hatimiliki ya kimila itakavyoboresha maisha yake mara baada ya
kupokea hatimiliki hiyo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero
iliyolenga kutoa hatimiliki za kimila na kuzindua jengo la masjala ya ardhi
lililojengwa na MKURABITA katika Halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment