Tarehe 04 Agosti, 2022
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imegusa maisha ya wananchi wa Kijiji cha Kitanga, wilayani Kisarawe mkoani Pwani kwa kujenga visima vya maji safi na salama vinavyotatua changamoto ya ukosefu wa maji iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa eneo hilo.
Akizungumza na wanachi wa Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe leo, Mhe. Ndejembi ameipongeza TASAF na wananchi wa Kijiji hicho kwa ushirikiano uliowezesha kukamilika kwa visima hivyo ambavyo hivi sasa vinatoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa eneo hilo.
Mhe. Ndejembi amewataka wananchi wa Kijiji hicho kuhakikisha wanavitunza visima hivyo ili viendelee kuwa msaada kwa wananchi wa eneo hilo kwa kipindi kirefu kama Serikali ilivyokusudia.
“Serikali imewajengea visima hivi, sasa ni jukumu lenu kuvitunza ili navyo vitutunze badala ya kuiachia TASAF na Serikali ya Kijiji jukumu hilo.” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, wanaojua umuhimu wa visima hivyo ni wananchi wa Kijiji cha Kitanga, hivyo Serikali haitofurahishwa kusikia baada ya miaka michache ijayo vimehaibika kwa kukosa matunzo.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Kitanga, Bi. Fatuma Bozi amesema kabla ya TASAF kuwajengea visima, walikuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwani walikuwa wakichota maji yaliyotuama ambayo yalikuwa yakitiririka kutoka bondeni, hivyo wanaishukuru Serikali kwa kuwajengea visima hivyo.
Mhe. Ndejembi amehitimisha ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF mkoani Pwani baada ya kutembelea Wilaya ya Bagamoyo na Kisarawe.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akichota maji kwenye kisima kilichojengwa na Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa ajili ya kuwahudumia wananchi mara baada ya
kukagua kisima hicho katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akimtwika ndoo ya maji mwananchi wa Kijiji cha Kitanga
wilayani Kisarawe mkoani Pwani mara baada ya kukagua kisima hicho kilichojengwa
na TASAF katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi akizungumza na walengwa wa TASAF wa na wananchi
wa Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe mara baada ya kukagua kisima
kilichojengwa na TASAF wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Wilaya ya Kisarawe.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akifuatilia taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini ya Kijiji cha Kitanga iliyokuwa ikiwasilishwa na Afisa Mtendaji wa
Kijiji hicho, Bw. Steven Michael wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo
iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani Kisarawe.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akimuelekeza jambo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa
TASAF, Bw. Msangi Tsetonga baada ya kukagua kisima kilichojengwa na TASAF
wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji
wa miradi ya TASAF wilayani Kisarawe.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akimsikiliza mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa
Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe, Bibi Hadija Shaka alipokuwa akitoa
ushuhuda wa namna alivyonufaika na TASAF wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu
Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani Kisarawe.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akipokelewa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
na wananchi wa Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe alipowasili katika kijiji
hicho akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
wilayani Kisarawe.
No comments:
Post a Comment