Na. James K.
Mwanamyoto-Morogoro
Tarehe 07 Agosti, 2022
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema walengwa wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini Manispaa ya Morogoro unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wamewezeshwa kuendesha mradi wa funza chuma kwa ajili ya kuzalisha chakula cha mifugo ambacho kinawaongezea kipato na kutatua changamoto ya upatikanaji wa chakula cha mifugo.
Mhe. Jenista amesema, kumekuwa na shida ya upatikanaji wa chakula cha mifugo hivyo mradi huo unaotumia teknolojia rahisi kuzalisha funza chuma kwa ajili ya chakula cha mifugo utatatua changamoto ya upatikanaji wa chakula cha mifugo kama ng’ombe, mbuzi, kuku, kondoo, samaki, bata na nguruwe.
“Mmesema hapa kupitia taarifa yenu kuwa, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kimefanya utafiti na kubaini kuwa funza chuma ni chakula kizuri cha mifugo kuliko vyakula vingine ambavyo vimekuwa vikitumika kulisha mifugo hivyo mradi huu ni mzuri na wa kimkakati ambao unapaswa kuendelezwa,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Mhe. Jenista ameongeza kuwa, mradi huo utasaidia kuhifadhi mazingira na kutatua changamoto ya uchafu wa mazingira katika masoko kwani badala ya takataka kutupwa hovyo ndani ya masoko, zitachukuliwa ili kuzalisha chakula cha mifugo na kuacha masoko yakiwa safi.
“Huu mradi ni suluhisho kubwa sana la changamoto
ya uchumi, uchafu wa mazingira na suala la ajira kwa makundi yote ya akina mama,
vijana na wenye ulemavu na walengwa wa TASAF, kwani ni mradi fungamanishi wenye
faida nyingi,” Mhe. Jenista amefafanua.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga amemshukuru Mhe. Jenista kwa kufanya ziara katika mradi huo wa funza chuma ambao una faida kubwa katika jamii, kwani utasaidia manispaa yake kuwa na mazingira safi na kuboresha maisha ya wananchi kwa kuwaongezea kipato.
Kutokana na faida ya uwepo wa mradi huo, Mhe. Kihanga amemhakikishia Mhe. Jenista kuwa, manispaa yake itawatumia Wahandisi waliopo kuwajengea walengwa wa TASAF na wananchi wengine vizimba vya kufuga funza chuma ili waweze kuzalisha kwa wingi chakula cha mifugo ambacho kitawaongezea kipato.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelekezo kwa Viongozi wa
Manispaa ya Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi ya
kukagua mradi wa kuzalisha funza chuma, unaotekelezwa na walengwa wa TASAF wa Kikundi
cha Faraja kilichopo katika Kata ya Mazimbu, Mtaa wa Mazimbu Darajani, Manispaa
ya Morogoro.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akizungumza na Viongozi wa Manispaa ya Morogoro na walengwa wa
TASAF wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa kuzalisha funza chuma,
unaotekelezwa na walengwa wa TASAF wa Kikundi cha Faraja kilichopo katika Kata
ya Mazimbu, Mtaa wa Mazimbu Darajani, Manispaa ya Morogoro.
Mlengwa
wa TASAF wa Kikundi cha Faraja, Kata ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro kinachojishughulisha
na mradi wa kuzalisha funza chuma, akionyesha namna wanavyotekeleza mradi huo
wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama iliyolenga kukagua mradi
huo katika Manispaa ya Morogoro.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga akimhakikishia Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama kuendeleza mradi wa funza chuma katika Manispaa ya Morogoro ili
kuinua uchumi wa wananchi wa Manispaa hiyo hususan walengwa wa TASAF, wanawake,
vijana na wenye ulemavu.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akifurahia jambo na mlengwa wa TASAF wa Kata ya Mazimbu,
Manispaa ya Morogoro, Bibi Schola Elias wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri
huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za TASAF, Manispaa ya Morogoro.
Mlengwa
wa TASAF wa Kata ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro, akielezea namna TASAF
ilivyomuwezesha kuboresha maisha yake wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za TASAF, Manispaa
ya Morogoro.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akizungumza na walengwa wa TASAF na wananchi wa Kata ya
Mazimbu, Manispaa ya Morogoro mara baada ya kukagua mradi wa funza chuma unaotekelezwa
na walengwa wa TASAF wa Kikundi cha Faraja cha Kata ya Mazimbu, Manispaa ya
Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za
TASAF.
No comments:
Post a Comment