Wednesday, June 3, 2026

KIKAO KAZI CHA WAKUU WA IDARA NA VITENGO VYA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALIWATU KATIKA WIZARA NA IDARA ZINAZOJITEGEMEA, WAKALA WA SERIKALI, TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA, SEKRETARIETI ZA MIKOA NA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MTAA

 

Kikao kazi cha siku tatu cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kinahitimishwa leo tarehe 3 Juni, 2026 jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray.

kikao hicho  kilifunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ambapo katika siku hizo tatu washiriki wamepewa uelewa wa namna ya kuimarisha utawala na usimamizi wa rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi, akizungumza na Wakuu wa Idara na vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wakati alipokuwa akiongoza majadiliano katika kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika Jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa Ofisi hiyo, SACP. Ibrahimu Mahumi


Washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa rasilimaliwatu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wawezeshaji mbalimbali leo tarehe 3 Juni, 2026 katika ukumbi wa Mabele Hall Jijini Dodoma.


Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa rasilimaliwatu leo tarehe 3 Juni, 2026 Jijini Dodoma


Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora wakifuatilia mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wawezeshaji wakati wa Kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa rasilimaliwatu leo tarehe 3 Juni, 2026 Jijini Dodoma


Washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa rasilimaliwatu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wawezeshaji mbalimbali leo tarehe 3 Juni, 2026 katika ukumbi wa Mabele Hall Jijini Dodoma.


Washiriki kutoka Sekretarieti Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wawezeshaji wakati wa Kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa rasilimaliwatu Jijini Dodoma.


Baadhi ya Wakurugenzi wasaidizi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora wakifuatilia mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wawezeshaji wakati wa Kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa rasilimaliwatu leo tarehe 3 Juni, 2026 Jijini Dodoma


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi, (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa Ofisi hiyo, SACP. Ibrahimu Mahumi

No comments:

Post a Comment