Thursday, June 18, 2026

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026

 Wananchi na Watumishi kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania wakiendelea kupata huduma katika mabanda ya maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma leo tarehe 18 Juni 2026.


Kupitia maadhimisho hayo, wananchi wanapata fursa ya kuhudumiwa papo kwa papo, kupata elimu kuhusu huduma za Serikali, kuwasilisha maoni yao na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu huduma za Umma.

Wananchi wote mnakaribishwa kutembelea viwanja vya maonesho ili kujionea huduma zinazotolewa na kunufaika na fursa ya kupata huduma kwa haraka na kwa urahisi kutoka kwa wataalamu wa wizara na Taasisi mbalimbali za umma.


















No comments:

Post a Comment