Monday, June 29, 2026

UZINGATIAJI WA ITIFAKI KATIKA UTUMISHI WA UMMA KUONGEZA UWAJIBIKAJI NA UADILIFU KIUTENDAJI

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Katibu Mkuu ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametoa rai kwa Watumishi wa Umma kuzingatia Itifaki katika Utumishi wa Umma ili kuongeza uwajibikaji na uadilifu kiutendaji kwa maslahi mapana ya Taifa.

Bw. Mkomi ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo katika eneo maalum la mafunzo kwa watumishi hao mara baada ya mkufunzi aliyekuwa akitoa mafunzo kuhusu Itifaki kuhitimisha mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa  kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa wa Itifaki katika Utumishi wa Umma.

Akiwasilisha mada kuhusu Itifaki, Mwezeshaji wa Mafunzo, Mhadhiri wa Diplomasia, kutoka Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, Bw. Lucas Humo amesema Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora ina majukumu mengi ikiwemo utoaji wa huduma mbalimbali za kiutumishi hivyo, ni muhimu kila mtumishi akajua wajibu wake ili aweze kuwahudumia Viongozi, Watumishi wa Umma na Wananchi kwa kuzingatia Itifaki mbalimbali zitakazosaidia kuonesha taswira nzuri ya ofisi.

Aidha, Bw. Humo amesema, Itifaki inahusisha namna inavyopaswa kuwasiliana, kushirikiana, na kufanya maamuzi kwa njia inayoheshimu sheria na taratibu zilizowekwa.

“Watumishi wa umma wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia uadilifu na uwazi kwa namna ya kuwasiliana, kushirikiana na kufanya maamuzi hivyo, wakifuata Itifaki na kuzitekeleza kwa ufanisi itaboresha utendaji kazi”, amesema Bw. Humo.

Bw. Humo, amewaasa watumishi hao kutunza taarifa za ofisi, kuzingatia muda wa kazi wakati wa kuingia na kutoka, kuwajali wageni wanapowasilisha masuala yao ya kiutumishi, kuzingatia mavazi wanapokuwa katika eneo la kazi pamoja na kuwatambua wageni wanapofika katika ofisi hiyo kwa vyeo vyao ili kutoa huduma kwa haki na usawa.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Mhadhiri wa Diplomasia, kutoka Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, Bw. Lucas Humo akifafanua jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu Itifaki wakati wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaliyolenga kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Wanaomsikiliza ni Wakurugenzi na Watumishi wa ofisi hiyo.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mada kuhusu Itifaki wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Viongozi, Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mada kuhusu Itifaki wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Mhadhiri wa Diplomasia, kutoka Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, Bw. Lucas Humo (kulia) akionyesha kwa vitendo Itifaki ya kusalimiana wakati wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaliyolenga kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, ambaye ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco Kipanda.


Sehemu ya Wakurugenzi na  Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mada kuhusu Itifaki wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Mtumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Joyce Atanas akiuliza swali kuhusu Itifaki mara baada ya Mhadhiri wa Diplomasia, Bw. Lucas Humo (hayupo pichani) kuwasilisha mada kuhusu Itifaki mbalimbali katika Utumishi wa Umma wakati wa mafunzo kwa watumishi wa ofisi hiyo yaliyolenga kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma


Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.



No comments:

Post a Comment