Na. Antonia Mbwambo- Mbeya
Tarehe 29
Juni, 2026
Serikali
imeendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa Watumishi wa Umma kupitia
utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi, hatua inayolenga kuongeza
ufanisi wa utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute,
wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba za watumishi katika Shule za Msingi
Ngolela, Wilaya ya Kyela na Idweli, Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya,
iliyohusisha wataalamu kutoka Ofisi hiyo pamoja na Watumishi Housing Investments
(WHI).
Bw.
Allute amesema makazi bora yataongeza ari ya kazi kwa Walimu na kuboresha
utoaji wa huduma. Aidha, amewataka Watumishi watakaonufaika na nyumba hizo
kuzitunza vizuri mara zitakapokamilika kwa kuwa ni mali za umma na zinazopaswa
kudumu ili kuwanufaisha Watumishi wa baadae.
"Serikali
inaendelea kuwekeza fedha nyingi katika kuboresha mazingira ya kazi kwa Watumishi
wa Umma, hivyo ni wajibu wa kila mnufaika kuhakikisha nyumba hizi zinatunzwa
vizuri mara zitakapokamilika na kuanza kutumika ili ziendelee kuhudumia
watumishi wa sasa na wa baadae," Bw. Allute amesema
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti, kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI,
Bi. Julieth Magambo, amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika ujenzi wa
nyumba za watumishi ili kuhakikisha wanapata mazingira bora, salama na yenye
utulivu yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Awali,
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ngolela, Bw. Samsoni Anyosisye, ameishukuru
Serikali kwa mradi huo, huku akieleza kuwa nyumba zilizopo zimechakaa na
hazifai kwa matumizi, hali iliyowalazimu Walimu wengi kuishi mbali na shule.
Naye
Mwalimu wa Shule ya Msingi Idweli, Bw. Tejile Mathew, amesema kukamilika kwa
nyumba hizo kutaleta motisha ya kazi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa
huduma ya Elimu.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyenyoosha mkono) akitaka ufafanuzi wa jambo wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Shule ya msingi Ngolela iliyopo Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti,Bi Julieth Magambo wa Ofisi hiyo.
Muonekano wa mbele wa jengo la
mradi wa makazi ya watumishi wa umma wa Shule ya msingi
Ngolela, iliyopo Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Ngolela, Bw. Samsoni Anyosisye (wanne kutoka kushoto) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Kitengo cha
Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (wa kwanza kutoka kulia) wakati wa ukaguzi
wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Shule ya msingi
Ngolela iliyopo Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya
Muonekano wa mbele wa jengo la
zamani walilokuwa wakiishi Waalimu wa shule ya msingi Ngolela iliyopo Kyela
Mkoani Mbeya kabla ya jengo hilo kuchakaa na kushindwa kutumika kwa makazi
Timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watumishi Housing
Investment (WHI) ikiwa katika picha ya pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Ngolela, Bw. Samsoni Anyosisye (wanne kutoka kushoto) mara baada ya timu
hiyo kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Shule ya
msingi Ngolela iliyopo Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya
Muonekano wa nyuma wa jengo la
zamani walilokuwa wakiishi Waalimu wa shule ya msingi Ngolela iliyopo Kyela
Mkoani Mbeya kabla ya jengo hilo kuchakaa na kushindwa kutumika kwa makazi
Timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watumishi Housing
Investment (WHI) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwalimu wa Shule ya Msingi
Idweli, Bw. Tejile Mathew pamoja na mafundi wanaosimamia mradi huo mara baada
ya timu hiyo kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa
Shule ya msingi Ngolela iliyopo Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya
Muonekano wa mbele wa jengo la
mradi wa makazi ya watumishi wa umma wa Shule ya msingi Idwelu,
iliyopo Wilaya ya Rugwe Mkoa wa Mbeya

No comments:
Post a Comment