Na Eric Amani
Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imeendelea na mazoezi yake katika jiji la Dodoma ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kushiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) mwaka 2025 ambayo yanatarajiwa kuanza mwezi Septemba 1.
Wachezaji wa timu hiyo wameonyesha ari na mshikamano mkubwa, wakilenga kufanya vizuri katika mashindano hayo yanayotarajiwa kukutanisha timu mbalimbali za watumishi wa umma kutoka wizara, idara na taasisi mbalimbali za serikali katika Jiji la Mwanza.
Mashindano ya SHIMIWI 2025 yamekuwa chachu ya kuimarisha afya za watumishi, kukuza vipaji na kuimarisha mshikamano kazini kupitia michezo ikiwemo mpira wa pete, riadha, mpira wa miguu na michezo mingine.
![]() |
| Sehemu ya Wachezaji wa Mpira wa Pete wa Ofisi ya Rais - UTUMISHI wakifanya mazoezi ya viungo ikiwa ni maandalizi ya kushiriki mashindano ya SHIMIWI 2025 jijini Mwanza |
![]() |
| Timu ya Mpira wa Pete Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika mechi ya mazoezi kwa ajili ya kujianda na mashindano ya SHIMIWI 2025 |
![]() |



No comments:
Post a Comment