Na
Eric Amani
Watumishi wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, leo Septemba 1, 2025 katika Mji wa Serikali Mtumba
jijini Dodoma wamepatiwa mafunzo ya kujitambua kwa lengo la kuongeza ufanisi
katika utendaji wa kazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa umma.
Akizungumza baada
ya kuhitimishwa kwa mafunzo hayo, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais – UTUMISHI,
Bw. Cyrus Kapinga ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera amesema
kuwa kujitambua ni msingi wa kila mtumishi kujua nafasi yake, uwezo wake na
wajibu wake katika kuwahudumia wananchi kwa weledi na uadilifu.
Mafunzo hayo ambayo hufanyika kila Jumatatu ya wiki yameelezwa
kuwa ni sehemu ya mkakati wa ofisi hiyo kuboresha utendaji kazi na kuwajengea
uwezo watumishi wa umma katika maeneo ya mawasiliano, uongozi, ubunifu na
uwajibikaji.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bi. Noela Bomani ameeleza
kuwa kujitambua sio nguzo muhimu ya mafanikio ya mtu binafsi tu, bali ni ya taasisi, kwani humsaidia mtumishi wa umma
kutambua nguvu na udhaifu wake, hivyo kuwezesha kufanya maamuzi sahihi ya
kikazi na kijamii.
Mafunzo hayo yametoa msisitizo katika maeneo ya
mawasiliano chanya, nidhamu ya kazi, kujenga mshikamano wa kikazi, ushirikiano
ikiwa pamoja na kukuza thamani ya Taifa na utu. Aidha, watumishi wametakiwa
kutumia uelewa walioupata ili kuongeza ari ya kufanya kazi kwa bidii, ubunifu
na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
![]() |
| Baadhi ya Watumishi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikilizia Mwezeshaji Bi Noela akitoa mafunzo juu ya akili hisia Leo Sepetemba 1, 2025. |
![]() |
| Mwezeshaji Bi. Noela Bomani Leo Septemba 1,2025 katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ametoa mafunzo kwa Watumishi wa Ofisi ya Rais - UTUMISHI juu ya Kujitambua "SELF AWARENESS". |
![]() |
| Baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifatilia kwa umakini mafunzo kutoka kwa Mwezeshaji Kuhusu Kujitambua Leo Septemba 1, 2025 katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. |
![]() |






No comments:
Post a Comment