Monday, September 8, 2025

TIMU YA MPIRA WA MIGUU OFISI YA RAIS - UTUMISHI YATINGA ROBO FAINALI.

 Na Eric Amani, Mwanza

Timu ya mpira wa miguu ya Ofisi ya Rais - UTUMISHI na Utawala Bora imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea jijini Mwanza.

UTUMISHI walipata nafasi hiyo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa uwanjani na kujikusanyia alama muhimu katika michezo ya hatua za makundi dhidi ya Timu ya Mahakama, hali iliyowafanya kufuzu na kuendelea na safari ya kuwania ubingwa wa mwaka huu 2025.

Mashindano ya SHIMIWI 2025 yamehusisha timu mbalimbali kutoka Wizara na Taasisi za Serikali kwa lengo la kujenga mshikamano na kudumisha afya za watumishi kupitia michezo ikiwa na kauli mbiu "Michezo kwa Watumishi, Huongeza Tija Kazini, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu".

Akizungumza mara baada ya mchezo uliowapa tiketi ya kuingia robo fainali, nahodha wa timu hiyo, Bw. Gimonge Chacha alisema “ushindi huo ni matokeo ya mshikamano, nidhamu ya hali ya juu na maandalizi ya muda mrefu”.

Timu ya Ofisi ya Rais - UTUMISHI sasa inajiandaa kukutana na wapinzani wao katika hatua ya robo fainali, huku wachezaji na mashabiki wakionyesha matumaini makubwa na timu yao kuwa itaendelea kufanya vizuri zaidi na hata kutwaa ubingwa wa SHIMIWI 2025.

Picha ya pamoja ya timu ya mpira wa miguu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa mashindano ya SHIMIWI 2025 Jijini Mwanza

Mchezaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw.Salum akijaribu kumtoka mchezaji wa timu ya Mahakama wakati wa mechi ya hatua ya mtuano kuwania nafasi ya kufuzu kwenda robo fainali katika mashindano ya SHIMIWI jijini Mwanza Sepemba 7, 2025
Wachezaji wa Ofisi ya Rais - UTUMISHI wakiwania mpira wa kona uliyopigwa wakati wa mechi dhidi ya timu ya Mahakama Septemba 7, 2025 UTUMISHI ilipata ushindi wa bao Moja na kutinga Robo Fainali katika mashindano ya SHIMIWI 2025, Mwanza 

Baadhi ya wachezaji wa timu ya mpira wa miguu Ofisi ya Rais -UTUMISHI wakifatilia kwa karibu mchezo wao dhidi ya Mahakama ambapo UTUMISHI iliibuka mshindi kwa kukushinda goli moja Septemba 7, 2025 Jijini Mwanza

Nahodha wa timu ya Ofisi ya Rais - UTUMISHI Bw. Gimonde Chacha akiwa katika mchezo dhidi ya timu ya Mahakama ambapo UTUMISHI ilishinda Goli Moja na kuelekea Robo fainali Jijini Dodoma


No comments:

Post a Comment