Monday, September 8, 2025

TIMU YA WANAWAKE YA RIADHA OFISI YA RAIS - UTUMISHI YAINGIA FAINALI KATIKA MBIO ZA KUPOKEZANA

Na Eric Amani, Mwanza

Timu ya wanawake ya riadha ya Ofisi ya Rais- UTUMISHI imefanikiwa kutinga hatua ya fainali katika mbio za kupokezana (relay) kwenye mashindano ya SHIMIWI kwa mwaka 2025 yanayoendelea jijini Mwanza.

Wanariadha wa Utumishi walionesha kasi ya hali ya juu katika mbio za nusu fainali, hatua iliyowapa tiketi ya moja kwa moja ya kucheza fainali, wakibeba matumaini ya kutwaa ubingwa wa mwaka huu.

Kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo, Bw. Hassan Shaibu, mafanikio hayo yametokana na nidhamu ya hali ya juu ya wachezaji, mazoezi ya mara kwa mara na umoja ndani ya kikosi, huku akibainisha kuwa morali ya ushindi imeendelea kuwa kubwa zaidi kadri mashindano yanavyosonga mbele.

Wanawake wa Utumishi sasa wanasubiri kumenyana na timu pinzani katika fainali ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkali, huku wakipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kutokana na kiwango walichokionyesha katika hatua zilizopita. 



Afisa Tawala Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi Yustina Dyabene akipasha viungo kabla ya kuanza mbio za kupokezana katika mashindano ya SHIMIWI 2025 Jijini Mwanza.


Bi Maria Musiba ambaye ni mtumishi wa Ofisi ya Rais - UTUMISHI akijianda kuanza mbio katika mchezo wa mbio za kupokezana kwenye mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea Jijni Mwanza.
Kwenye Picha ni wachezaji wa timu ya riadha kutokea ofisi ya Rais - UTUMISHI wakifurahia ushindi uliyowapelekea kuingia fainali za mbio hizo Leo septemba 8, 2025 Jijini Mwanza.


No comments:

Post a Comment