Na. Antonia Mbwambo- Dodoma
Tarehe 22.09.2025
Ili kuhakikisha takwimu za mahitaji ya watumishi katika taasisi za umma zina uhalisia utakaowezesha maamuzi mbalimbali kuhusiana na rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeandaa mikakati itakayoboresha utekelezaji wa Mfumo wa e-Msawazo ikiwemo kujadili na kukubaliana na wadau wa Mfumo kuhusu vigezo vitakavyotumika katika kutathmini mahitaji ya watumishi zikiwemo Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Hayo yamesemwa leo tarehe 22.09.2025 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji wakati akimwakilisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI kufungua kikao kazi cha siku mbili cha wadau kujadili vigezo vitakavyotumika katika kusafisha takwimu za mahitaji ya Watumishi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Bw. Ngangaji amesema, Ofisi ya Rais-UTUMISHI inaendelea kuchukua hatua na kuhakikisha Mfumo wa e-Msawazo unaendelea kuwa nyenzo itakayowezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi za Watumishi waliopo na wanaohitajika kwa masilahi ya taifa.
“Mfumo wa e-Msawazo unaendelea kuboreshwa ili taarifa zinazopatikana kupitia Mfumo zinaendelea kuwa sahihi zaidi kuwezesha maamuzi mbalimbali ya usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.” Amesisitiza Bw. Ngangaji.
Bw. Ngangaji amewaelekeza washiriki wa kikao kazi hicho, kutumia vizuri fursa hiyo ili kupata vigezo vitakavyokubalika kufanya tathmini ya mahitaji vitakavyotumika katika zoezi la kusafisha taarifa kwenye Mfumo wa e-Msawazo katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na kufanya e-Msawazo inakuwa na tija.
Akitoa neno la utangulizi, Mkurugenzi wa Uendelezaji Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda amesema kikao kazi hicho ni mahususi kwa ajili ya wadau ili waweze kujadili tathmini ya mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kupata maoni toka kwa wadau hao na kuboresha mfumo huo katika Utumishi wa Umma kwa masilahi mapana ya taifa.
“Tumepata matokeo ya tathmini, sasa kabla ya kuendelea na mchakato mwingine, tumeona ni vema tukakutana na wadau hawa, tumeanza na wadau wa OR -TAMISEMI kutokana na uwingi wa uwakilishi wao katika Utumishi wa Umma.” Ameongeza Bw. Kipanda
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki, Mwenyekiti wa kikao kazi hicho ambaye ni Afisa Rasilimaliwatu, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Bw. Shaban Duru ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa ili kupata matokeo tarajiwa kama ilivyokusudiwa.
Mgeni Rasmi
Bw. Cosmas Ngangaji(aliyeshika daftari na Faili) akiwasili katika Ukumbi wa
NAOT katika ufunguzi wa kikao kazi cha siku mbili cha wadau kujadili vigezo
vitakavyotumika katika kusafisha takwimu za mahitaji ya Watumishi wa
Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas
Ngangaji akitoa
hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi cha siku mbili cha wadau kujadili
vigezo vitakavyotumika katika kusafisha takwimu za mahitaji ya Watumishi wa
Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Ofisi za NAOT jijini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Uendelezaji Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda Ofisi ya Rais UTUMISHI, akitoa neno
la utangulizi katika kikao kazi cha siku mbili cha
wadau kujadili vigezo vitakavyotumika katika kusafisha takwimu za mahitaji ya
Watumishi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kabla ya
mgeni rasmi kufungua kikao hicho leo jijini
Dodoma.
Mgeni Rasmi
ambaye ni Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji
akitia saini kwenye kitabu cha wageni katika Ofisi za NAOT Jijini Dodoma mara
baada ya kuwasili katika Ofisi hizo kwa lengo la kufungua kikao kazi cha siku mbili cha wadau kujadili vigezo vitakavyotumika katika
kusafisha takwimu za mahitaji ya Watumishi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka
za Serikali za Mitaa
Wakurugenzi
kutoka Ofisi ya Rais,UTUMISHI, wakipata picha ya pamoja
na Mgeni Rasmi Bw. Cosmas Ngangaji ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Mipango
katika Ofisi hiyo mara baada ya kufungua kikao kazi cha siku mbili cha wadau
kujadili vigezo vitakavyotumika katika kusafisha takwimu za mahitaji ya
Watumishi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa jijini
Dodoma
Baadhi wa
wakurugenzi na washiriki wengine, wakifuatilia kikao kazi cha e- Msawazo wakati
Mgeni Rasmi alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao hicho.
Wakurugenzi
wasaidizi pamoja na wawezeshaji wa kikao kazi cha siku mbili cha wadau kujadili
vigezo vitakavyotumika katika kusafisha takwimu za mahitaji ya Watumishi wa
Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakiwa katika picha ya
pamoja na Mgeni Rasmi mara baada ya Mgeni Rasmi kufungua kikao hicho.
Washiriki kutoka Sekretarieti za Mikoa pamoja na Halmashauri ya jiji wakipata picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Bw. Cosmas Ngangaji mara baada ya kufungua kikao kazi cha siku mbili cha wadau kujadili vigezo vitakavyotumika katika kusafisha takwimu za mahitaji ya Watumishi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa jijini Dodoma
Wadau
kutoka Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakifuatilia kikao
kazi cha e- Msawazo kilichofanyika katika Ofisi za NAOT jijini Dodoma.
Wadau kutoka Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakifuatilia kikao kazi cha e- Msawazo kilichofanyika katika Ofisi za NAOT jijini Dodoma.
Washiriki kutoka Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakifuatilia kikao kazi cha e- Msawazo kilichofanyika katika Ofisi za NAOT jijini Dodoma.













No comments:
Post a Comment