Na Veronica Mwafisi na Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe 01 Septemba, 2025
Waratibu wa Jinsia Mahali pa
Kazi katika Utumishi wa Umma wametakiwa kutoa elimu kwa watumishi wa umma kupitia
Wizara zao juu ya namna ya kukabiliana na vikwazo wanavyokutana navyo katika
maeneo yao ya kazi ikiwemo uonevu na dhuluma.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI,
Bw. Cyrus Kapinga alipokuwa akimwakilisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI kufungua
kikao
kazi kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa
mipango kazi ya ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa fedha 2024/25 jijini Dodoma.
Bw.
Kapinga amesema kuna changamoto ya jinsi ya kutoa taarifa kwani taarifa nyingi
hazina maudhui ambayo mtu anaweza kupata picha ya ujumuimuishaji wa masuala ya
jinsia katika Utumishi wa Umma.
Aidha,
Bw. Kapinga amewataka waratibu hao kutumia kikamilifu muda na nafasi waliyopatiwa
na waajiri wao katika kuwasilisha utekelezaji wa mpango kazi kwa weledi na
ufasaha pamoja na kupokea maoni na ushauri wa namna bora ya utekelezaji kwa
Mwaka wa fedha 2025/26.
Kadhalika, Bw. Kapinga
ameishukuru Taasisi ya UONGOZI kwa
kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali kuhusu programu za Uongozi kwa Wanawake
awamu kwa awamu na kuwezesha kufanyika kwa Semina mbalimbali za mwongozo wa
ujumuishwaji wa Jinsia katika Utumishi wa Umma kwa Ngazi ya Wizara.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza,
Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo amewaasa Waratibu hao kuhakikisha wanatekeleza
miongozo mbalimbali inayohusu ujumuishwaji wa jinsia mahali pa kazi
kwa ufanisi kama
ilivyokusudiwa na Serikali.
Akitoa neno la shukrani kwa
niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Kaimu Mkuu wa Idara ya
Tafiti na Sera, Bi. Carolina Israel amesema, Ofisi ya Rais-UTUMISHI imekuwa
ikitoa ushirikiano mkubwa wakati wa mafunzo mbalimbali ya ujumuishwaji wa
jinsia mahali pa kazi katika Utumishi wa Umma hivyo, Taasisi ya UONGOZI
itaendelea kushirikiana na ofisi hiyo katika kutoa mafunzo hayo kwa ustawi wa
maendeleo ya taifa.
Kikao kazi cha Waratibu wa jinsia Mahali pa Kazi katika Utumishi wa Umma
kinafanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 01 hadi 02 Septemba, 2025
katika Ukumbi wa Lounge uliopo katika hoteli ya St. Gaspar jijini Dodoma.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera
wa ofisi hiyo, Bw. Cyrus Kapinga akizungumza
na Waratibu wa Jinsia Mahali Pa Kazi Ngazi ya Wizara
katika Utumishi wa Umma wakati wa kikao kazi kilicholenga kupokea taarifa
ya utekelezaji wa mipango kazi ya ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa fedha
2024/25 kilichofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Waratibu
wa Jinsia Mahali Pa Kazi Ngazi ya Wizara katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Mwakilishi
wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera
wa ofisi hiyo, Bw. Cyrus Kapinga wakati
akifungua kikao kazi kilicholenga kupokea
taarifa ya utekelezaji wa mipango kazi ya ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa
fedha 2024/25 kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza,
Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo (kulia) akifuatilia mada mbalimbali
wakati wa kikao kazi kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa mipango
kazi ya ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa fedha 2024/25 kilichofanyika jijini
Dodoma. Kulia kwake ni Afisa Mipango Mwandamizi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw.
Staricko Nyikwa.
Mkurugenzi
Msaidizi, Idara
ya Usimamizi wa Rasilimawatu Serikalini, Bi. Jeanfrida Mushumbushi
(katikati) akielezea
ujumuishwaji wa jinsi unavyotumika katika Idara hiyo wakati wa kikao
kazi kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa mipango kazi ya
ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa fedha 2024/25 kilichofanyika jijini Dodoma.
Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Maafisa Waandamizi, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Jafari Maganga na kushoto kwake ni Mkurugenzi
Msaidizi, Idara ya Mipango, Bw. Bonaventure Amri.
Afisa Tawala Mkuu, Wizara ya Maji, Bi. Suzana
Mutagahywa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa jinsia ya Wizara hiyo wakati
wa kikao kazi kilicholenga
kupokea taarifa ya utekelezaji wa mipango kazi ya ujumuishwaji wa jinsia ya
Mwaka wa fedha 2024/25 kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi-Taasisi ya UONGOZI ambaye ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Tafiti na Sera, Bi. Carolina Israel akitoa neno la shukrani kwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera wa ofisi hiyo, Bw. Cyrus Kapinga mara baada ya Mkurugenzi huyo kufungua rasmi kikao kazi kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa mipango kazi ya ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa fedha 2024/25 kilichofanyika jijini Dodoma.
Afisa Tawala, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bw. Beatus Wenga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa jinsia ya Wizara hiyo wakati wa kikao kazi kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa mipango kazi ya ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa fedha 2024/25 kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera wa ofisi hiyo, Bw. Cyrus Kapinga (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Waratibu wa Jinsia Mahali Pa Kazi Ngazi ya Wizara katika Utumishi wa Umma mara baada ya kufungua kikao kazi kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa mipango kazi ya ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa fedha 2024/25 kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera
wa ofisi hiyo, Bw. Cyrus Kapinga
(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi
wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI mara baada ya kufungua kikao
kazi kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa mipango kazi ya
ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa fedha 2024/25 kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili, Ofisi Rais- UTUMISHI, Bi. Felister (kushoto) akifafanua jambo kuhusu ujumuishwaji wa jinsi unavyotumika katika Idara hiyo wakati wa kikao kazi kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa mipango kazi ya ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa fedha 2024/25 kilichofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bi. Leila Mavika.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera
wa ofisi hiyo, Bw. Cyrus Kapinga
(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi
Wasaidizi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI mara baada ya
kufungua kikao kazi kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa mipango kazi
ya ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa fedha 2024/25 kilichofanyika jijini
Dodoma.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera
wa ofisi hiyo, Bw. Cyrus Kapinga
(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wawezeshaji katika kikao
kazi kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa mipango kazi ya
ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa fedha 2024/25 kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mary Mwakapenda (kulia) akijadili jambo na Mratibu wa Mafunzo kutoka Taasisi ya UONGOZI, Bw. Zefania Mkingi (kushoto) kabla ya kuanza kwa kikao kazi kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa mipango kazi ya ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa fedha 2024/25 kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera
wa ofisi hiyo, Bw. Cyrus Kapinga
(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti
kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa kushirikiana na Taasisi ya UONGOZI iliyoandaa
kikao kazi kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa
mipango kazi ya ujumuishwaji wa jinsia ya Mwaka wa fedha 2024/25 kilichofanyika
jijini Dodoma.

No comments:
Post a Comment