Na Eric Amani, Uwanja wa Kirumba Mwanza
Timu ya riadha ya wanawake ya Ofisi ya Rais - UTUMISHI imeibuka
kidedea leo tarehe 11 Septemba, 2025 baada ya
kutwaa ubingwa wa mbio za kupokezana (relay) katika mashindano ya Shirikisho la
Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea katika Uwanja wa
CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wanariadha wa Utumishi walionesha uwezo mkubwa na mshikamano wa kiufundi
uliopelekea kushinda kwa kishindo na kuwapiku wapinzani wao waliokuwa wakipewa
nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo.
Ushindi
huu unaongeza heshima kwa Utumishi, ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika
michezo mbalimbali, ikiwa ni kielelezo cha juhudi za kujenga mshikamo na afya
bora kwa watumishi wa umma kupitia michezo.

No comments:
Post a Comment