Na Antonia Mbwambo-Mwanza
Kamati ya kitaifa
ya kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza (MSY) mahali pa kazi
katika Utumishi wa Umma ambayo inajumuisha Waratibu ngazi ya halmashauri, mkoa
na kitaifa, imetakiwa
kuimarisha malengo ya kudhibiti magonjwa hayo kwa kuhakikisha Wizara,
Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinasimamia utekelezaji
wa Mwongozo wa kudhibiti
VVU, UKIMWI na MSY na uwasilishwaji wa
taarifa kwa wakati .
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Musa Magufuli kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika ufunguzi wa kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 ngazi ya Mkoa na Taifa.
Bw. Magufuli amesema, ili kufikia malengo ya kudhibiti magonjwa
hayo, mafunzo ya kuwajengea watumishi uwezo wa namna ya
kudhibiti yanatakiwa kutolewa na kuteua Kamati za Kudhibiti VVU, UKIMWI na MSY
katika utumishi wa Umma.
Aidha, Bw. Magufuli, amesema kwa kutambua umuhimu wa Afya na Ustawi wa Watumishi wa Umma nchini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI iko katika hatua za mwisho za kukamilisha Mwongozo na Waraka kuhusu kudhibiti VVU, UKIMWI na MSY ikiwemo na changamoto za Afya ya Akili mahali pa kazi katika Utumishi wa Umma.
Bw. Magufuli amewashukuru na kuwapongeza wakuu wa Taasisi za umma nchini kwa kutekeleza kikamilifu afua za kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa na kusisitiza kuwa Ofisi ya Rais-UTUMISHI itaendelea kufanya ufuatiliaji kwa lengo la kubaini mafanikio na changamoto za utekelezaji.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Bw. Balandya Elikana,
ametoa rai
kwa kila halmashauri kendelea kutekeleza Mwongozo wa VVU, UKIMWI na Magonja
Sugu Yasiyoambukiza (MSY) mahali pa kazi katika Utumishi wa Umma kwa masilahi
mapana ya taifa.
Mkurugenzi wa Idara ya
Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Bw. Musa Magufuli akitoa hotuba ya Mgeni Rasmi katika kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa
Afua za VVU, UKIMWI na Magonjwa yasiyoambukiza kwa kipindi cha robo ya kwanza
ya mwaka wa fedha 2024/25
Katibu Tawala Mkoa Bw. Balandya Elikana akizungumza na waratibu wa Kitaifa(pichani hawapo) katika kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za VVU,UKIMWI na Magonjwa yasiyoambukiza kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/25
Mkurugenzi Msaidizi Anuai za
Jamii na Mratibu wa VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo akiwasilisha mada kuhusu Mwongozo
wa kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza (MSY) mahali pa kazi katika
utumishi wa umma wakati wa kikao kazi cha kupokea
taarifa ya utekelezaji wa Afua za VVU, UKIMWI na Magonjwa yasiyoambukiza kwa
kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/25 Jijini Mwanza
Mkurugenzi msaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu,Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Bw. Deodatus Mwiliko (wa kwanza kulia) akifuatilia kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za VVU, UKIMWI na Magonjwa yasiyoambukiza kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/25 Jijini Mwanza
Baadhi ya waratibu Kamati ya Mkoa (waliosimama)wakipata picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Bw. Musa Magufuli, baada ya kufungua kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za VVU, UKIMWI na Magonjwa yasiyoambukiza kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/25 Jijini Mwanza, kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo na kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana.
Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu
wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi.
Mwanaamani Mtoo (kushoto) akifuatilia mada mbalimbali
wakati wa kikao kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za
VVU, UKIMWI na Magonjwa yasiyoambukiza.
Mratibu wa Kamati Mkoa Bi. Ramla Juma Phroi akifuatilia
mada mbalimbali wakati wa kikao kazi cha kupokea
taarifa ya utekelezaji wa Afua za VVU, UKIMWI na Magonjwa yasiyoambukiza.
Baadhi ya wajumbe wa sekretarieti (waliosimama) wakipata picha ya Pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Bw. Musa Magufuli katika kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za VVU, UKIMWI na Magonjwa yasiyoambukiza.
Waratibu wa Kitaifa wakitambulishwa mbele ya Mgeni Rasmi kabla ya kufungua kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za VVU, UKIMWI na Magonjwa yasiyoambukiza.
Baadhi ya waratibu wa Wizara (waliosimama)wakipata
picha ya Pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa
Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Bw. Musa Magufuli(wa tatu kulia
aliyekaa) baada ya kufungua kikao kazi cha kupokea taarifa ya
utekelezaji wa Afua za VVU,UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza jijini Mwanza.
Waratibu wa kitaifa wakisikiliza hotuba iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Bw. Musa Magufuli kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za VVU, UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza jijini Mwanza.
Baadhi ya waratibu wa Wizara (waliosimama)wakipata picha ya Pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Bw. Musa Magufuli(wa tatu kulia aliyekaa) baada ya kufungua kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za VVU,UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza jijini Mwanza.
Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo akitoa kwa ufupi maneno ya utangulizi Kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana katika Ofisi yake kabla ya ufunguzi wa kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za VVU,UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza jijini Mwanza.
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Utawala na
Usimamizi wa Rasilimali Watu Bw. Daniel Machunda akiahirisha kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za VVU,
UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw.
Balandya Elikana jijini Mwanza.














No comments:
Post a Comment