Na Antonia Mbwambo- Dodoma
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wamekumbushwa juu ya kuzingatia Kanuni za Maadili zinazowaongoza katika utendaji wao kwa kufuata Sera, Sheria na Taratibu zilizopo ili kuleta tija kwa maslahi mapana ya Taifa.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais - UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli ameyasema hayo leo tarehe 15 Septemba, 2025 alipokuwa akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma baada ya mwezeshaji kuhitimisha mafunzo ambayo hufanyika mwanzoni mwa kila wiki.
Bw. Magufuli amesema,ni vyema watumishi kuwajibika kwa umma kwa kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma bora na kwa wakati bila kujali uhusiano uliopo kati ya mtumishi na mwananchi anayepewa huduma.
Awali, akitoa mafunzo hayo, Afisa Habari Mkuu Idara ya Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Bw. Rocky Setembo amesema, Kanuni hizo ndizo zinazomuongoza mtumishi juu ya tabia na mwenendo mwema wa kuzingatia ili kuleta matokeo chanya katika utoaji wa huduma.
Bw. Setembo ameongeza kuwa,
kwa kufuata kanuni hizo kutamuwezesha mtumishi wa umma kuepuka viashiria
vyovyote vitakavyosababisha uvunjifu wa amani na kuwa mfano bora wa kuigwa
katika jamii inayomzunguka.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Bw. Musa Magufuli akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo baada ya Mwezeshaji kuhitimisha mafunzo katika mji wa Mtumba Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakiendelea kutolewa katika Ofisi hizo zilizopo mji wa Mtumba Dodoma.
Afisa Habari Mkuu, Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Rocky Setembo akisisitiza jambo alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na mtumishi kuhusu Kanuni za Maadili ya utendaji katika utumishi wa umma yaliyofanyika katika Ofisi hiyo iliyopo mji wa mtumba Dodoma.
Afisa
Habari Mkuu, Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Rocky Setembo akitoa mafunzo kuhusu
Kanuni za Maadili ya utendaji katika utumishi wa umma yaliyofanyika katika
Ofisi hiyo iliyopo mji wa mtumba Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI
Bw. Musa Magufuli (wa kwanza mbele) akifurahia jambo pamoja na watumishi wengine wa Ofisi hiyo
wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakiendelea katika mji wa Mtumba Dodoma.
Baadhi
ya wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora pamoja na watumishi wengine wakifurahia jambo walipokuwa wakifuatilia
mafunzo yaliyokuwa yakiendelea kutolewa katika Ofisi hizo zilizopo mji wa
Mtumba Dodoma.






No comments:
Post a Comment