Na. Veronica Mwafisi-Singida
Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments
ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute imekagua maendeleo ya mradi
wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma kwa upande wa elimu yanayojengwa
katika Kijiji cha Maluga, Halmashauri ya Wilaya ya
Iramba, mkoani Singida uliofikia 70% ambapo ukikamilika rasmi utawasaidia watumishi
hao kuwa karibu na ofisi wanazofanyia kazi kwa lengo la kutekeleza majukumu yao
kikamilifu.
Mara baada ya kukagua mradi huo leo, Kaimu Mkurugenzi Allute amesema,
kuna umuhimu wa makazi ya watumishi wa umma kuwa karibu na ofisi kwani
itaongeza tija ya utendajikazi serikalini.
“ujenzi huu wa makazi ya watumishi wa umma una umuhimu sana kwani utasaidia
kuongeza utendajikazi kwa watumishi wa eneo hili, lakini pia utasaidia kuepeukana
na changamoto ya makazi ambayo imekuwa ikiwakabili watumishi hao na kushindwa
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi,” amesema Mkurugenzi Allute
Vilevile, timu hiyo imekagua maendeleo ya ujenzi wa makazi ya
watumishi wa umma kwa upande wa afya katika Kijiji cha Makunda Halmashauri ya
Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti,
Bi. Julieth Magambo amewasisitiza Watumishi Housing Investments (WHI) ambao
ndio kandarasi inayojenga makazi katika mradi huo kuhakikisha wanakamilisha
miradi hiyo kwa wakati ili kuendana na mipango na bajeti ya Serikali.
Naye, Mhandisi Salum Chanzi kutoka WHI, ameahidi kukamilika kwa
wakati mradi huo ili kufikia malengo ya Serikali katika kuwatengenezea
mazingira bora watumishi wa umma.
Kwa upande wake, Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya fedha,
Bw. Ezekiel Odipo ameeleza kuwa, Serikali inatoa fedha nyingi ili kutimiza malengo
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya
kuongeza tija kwa watumishi wa umma ili waweze kutoa
huduma bora kwa maendeleo ya taifa.
Mradi wa ujenzi wa makazi hayo ya watumishi wa umma upo katika
hatua ya majaribio ambayo unatekelezwa kwenye mikoa ya Dodoma, Lindi, Singida,
Pwani na Ruvuma.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute
(wapili kutoka kulia) akizungumza jambo wakati akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma unaojengwa
katika Kijiji cha Maluga, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute
(wakwanza kulia) akielekea kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa makazi ya
Watumishi wa Umma unaojengwa katika Kijiji cha Maluga, Halmashauri ya Wilaya ya
Iramba, mkoani Singida. Kulia kwake ni Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara
ya fedha, Bw. Ezekiel Odipo.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute
(aliyenyoosha mkono) akisisitiza jambo wakati akikagua maendeleo ya mradi wa
ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma unaojengwa katika Kijiji cha Maluga,
Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, mkoani Singida. Wengine ni maafisa kutoka
Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments.

Mtaalam wa ujenzi kutoka WHI, Bw. Bazir Ndonde (wapili
kutoka kushoto) akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma kwa timu ya
wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments unaojengwa katika Kijiji cha
Maluga, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Mwonekano wa jengo la mradi wa makazi ya watumishi wa
umma lililopo katika Kijiji cha Maluga,
Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
No comments:
Post a Comment