HABARI KATIKA PICHA
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyenyoosha mkono) akizungumza jambo na Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi kutoka Wizara ya fedha, Bw.
Ezekiel Odipo (wakwanza kushoto) wakati wa ziara ya kikazi iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa
umma katika Shule
ya Sekondari Lumuma Green, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mwonekano wa jengo la mradi wa makazi ya watumishi wa
umma lililopo katika Shule ya Sekondari Lumuma Green, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
mkoani Dodoma.
Fundi mkuu anayejenga makazi ya watumishi wa umma, katika
Shule ya Msingi Chaludewa, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Fadhili
Kabainda (wapili kutoka kulia) akifafanua jambo kwa Mhandisi Salum Chanzi kutoka Watumishi Housing Investments
(wakwanza kulia) wakati wa ziara ya timu ya
wataalam kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na
Watumishi Housing Investments
iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma katika
Halmashauri hiyo mkoani Dodoma.
Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments ikijadili jambo wakati wa ziara ya kikazi iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa
umma katika Shule ya Sekondari Lumuma Green,
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mwonekano wa jengo la mradi wa makazi ya watumishi wa
umma lililopo katika Shule ya Msingi Chaludewa, kijiji cha Mlunduzi, Halmashauri ya
Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (wakwanza kulia) akisisitiza jambo kwa Mtakwimu
Mwandamizi Bw. Ombeni Kasayo (wapili kutoka kushoto) na Mchumi Mwandamizi
kutoka Watumishi Housing Investments, Bw. Damian Mnenwa (wakwanza kushoto) mara
baada ya timu ya wataalam kutoka Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na WHI kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya
watumishi wa umma katika Kijiji cha Ludewa,
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment