Na. Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango
wa kada ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka katika ustawi wa utumishi
wa umma huku akiahidi wakati wote Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora
itaendelea kutoa ushikiano kwa kada hiyo ili kuendelea kufanikisha
masuala mbalimbali ya kiutumishi.
⁹Mhe Simbachawene
ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam kwenye Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama
Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) kabla ya kumkaribisha Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa kwa ajili ya
kufungua Mkutano huo.
Amesema mikutano
hiyo ya Kitaaluma imekuwa ikileta tija kwa Wanataaluma hao kwani mbali ya
kupata maarifa bali wamekuwa wakibadilishana mawazo ya namna bora ya
kuboresha utendaji kazi wao
Ameongeza kuwa
" Mikutano hii ni muhimu kwao kwani imekuwa ikitoa dira kwa
Wanataaluma namna ya kutumia mifumo ya TEHAMA katika kazi zao za kila
siku badala ya utaratibu wa ubebaji wa mafaili uliokuwa ukifanyika hapo awali
"
Aidha,
Mhe.Simbachawene amewataka Wanachama hao kufanya kazi kwa bidii na kujiongezea
maarifa ili kuendana na mabadiliko ya TEHAMA yanatokea katika utendaji
kazi wao wa kila siku huku akiwataka Waajiri kuhakikisha wanakuwa msaada katika
kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.
Wakati huo huo,
Waziri Simbachawene amesema kuwa Serikali imeendelea kutoa ajira kwa watumishi
wa umma wakiwamo watunza kumbukumbu. Katika mwaka 2024-2025 kada hii tu ajira
mpya zilizotolewa ni 965 waliopandishwa cheo ni 1,237, kuwabadilishia kada
watumishi 59 (Recategorization) pamoja na kulipa malimbikizo ya mishahara kiasi
cha shilingi milioni 204.6
Katika hatua
nyingine, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora imeahidi
kuchangia kiasi cha Shilingi Mil.10 ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya
kuwezesha ujenzi wa Kituo cha Maarifa kitakachokuwa na masijala ya mfano, kumbi
za mikutano pamoja na ofisi za TRAMPA kinachotarajiwa kujengwa jijini Dodoma.
Akizungumza mara
baada ya kutoa ahadi hiyo, Mhe.Simbachawene amesema kimsingi kazi hiyo ya
ujenzi wa Kituo Maalum cha Maarifa cha TRAMPA kilipaswa kujengwa na
Serikali hivyo wao kama Ofisi yenye dhamana ya kusimamia Watumishi wa Kada hiyo
imeamua kuwa mstari wa mbele kuchangia kiasi hicho
Naye, Katibu Mkuu,
UTUMISHI, Bw .Juma Mkomi ameahidi kutoa Sh.milioni 10 kwa niaba ya timu
Menejimenti ya Ofisi hiyo ili kuhakikisha maono ya kujenga Kituo hicho cha
Maarifa yanatimia.
Awali, Mwenyekiti
wa TRAMPA, Devota Mrope amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika sekta mbalimbali
iliwemo katika kada ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka.
Rais Dkt. Samia
amekuwa mwana TRAMPA namba moja, amepigania maslahi ya watumishi wa umma
ikiwemo sisi mwana TRAMPA, ametoa ajira nyingi katika kipindi kifupi
ikiwemo kwa wanataaluma wa kada hii ya Menejimenti ya kumbukumbu na
nyaraka, amefanyia kazi changamoto zetu kwa kiasi kikubwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe.Kassim Majaliwa akikabidhiwa mfano wa funguo ya gari la wagonjwa kutoka
kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene lililotolewa na Chama Menejimenti ya
Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni zawadi ya kutambua mchango wake kwa wanachama
wa TRAMPA mara baada ya
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akifungua
Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka (
TRAMPA ) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza wakati
akifungua Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na
Nyaraka ( TRAMPA ) uliofanyika leo jijini Dar es SalaamWaziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George
Simbachawene akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama Menejimenti ya
Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa kufungua Mkutano huo uliofanyika
leo jijini Dar es Salaam
Sehemu ya Wanachama wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) Wwakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa kufungua Mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) Bi. Devotha Mrope akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) kabla ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa kufungua Mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment