Wednesday, September 18, 2019

SERIKALI YAFANYA MKUTANO WA USHAWISHI NA UTETEZI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA NGAZI YA WIZARA

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu Wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Philibert Kawemama akifungua mkutano kuhusu ushawishi na utetezi wa masuala ya watu wenye ulemavu katika ngazi ya wizara uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Utawala, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Bi. Mwanaheri Cheyo. 

Washiriki wa mkutano kuhusu ushawishi na utetezi wa masuala ya watu wenye ulemavu katika ngazi ya wizara wakifuatilia mada katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Bi.Ummy Nderiananga (kushoto) akiwasilisha  mada wakati wa mkutano kuhusu ushawishi na utetezi wa masuala ya watu wenye ulemavu katika ngazi ya wizara uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Agnes Meena (kushoto) akichangia  mada wakati wa mkutano kuhusu ushawishi na utetezi wa masuala ya watu wenye ulemavu katika ngazi ya wizara uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika akitoa ufafanuzi kuhusu ushawishi na utetezi wa masuala ya watu wenye ulemavu katika ngazi ya wizara kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment