Na. Lusungu Helela - ARUSHA.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema Serikali ya Tanzania imejipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu unakuwa huru, wa haki, uwazi na kuaminika.
Mhe.
Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 8, 2025 jijini
Arusha wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa
Wanasheria unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo.
Amesema katika kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, unakuwa wa amani, huru, wa haki na unaoaminika,
Serikali imechukua hatua mbalimbali zikiwemo kufanya Mapitio ya Sheria za Uchaguzi, Kuimarisha
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kutoa Elimu ya Mpiga Kura, Kuhakikisha
Usalama na Amani, Kujenga Maridhiano ya Kisiasa, Kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura; kifungu cha 16(5)
cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024
kinachoipa Tume jukumu la kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili
mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya uteuzi wa wagombea kwa uchaguzi mkuu
unaofuata.
Amesema
uchaguzi ni suala la Kikatiba na Kisheria huku akisisitiza kuwa Chama Cha
Wanasheria Tanganyika (TLS) ni Wakili wa Wananchi hivyo kina
dhamana kwa Taifa kusaidia wananchi kuelewa umuhimu wa uchaguzi na kuwa ushiriki wa kila Mtanzania
katika uchaguzi ni suala la kikatiba kupitia Ibara ya 5(1) ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania pia ni utekelezaji wa Ibara ya 8 ya Katiba kwa kuwa
mamlaka ya utawala yanatoka kwa wananchi.
“TLS
ni chombo cha Umma hivyo Mawakili mna nafasi ya kipekee ya kuhakikisha
wananchi wanapata haki ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu
huku kukiwa na mazingira bora kwa pande zote” Mhe. Simbachawene
amesisitiza.
Amesema TLS imekuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha haki, kutoa
msaada wa kisheria kwa wananchi, na kufuatilia mienendo ya uchaguzi na kuongeza
kuwa Serikali inatambua juhudi zao katika kutoa elimu ya mpiga kura na
kushiriki katika uangalizi wa kisheria wakati wa chaguzi”.
Ametoa wito kwa TLS kuendelea kushirikiana na Serikali, hasa kwa kutoa
mapendekezo ya kisheria kuhusu marekebisho ya sheria za uchaguzi, kutathmini
utekelezaji wa sheria hizo, na kuhakikisha kuwa sauti za wananchi zinasikika
kwa njia ya haki.
Kwa
upande wake, Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Mhe. Boniphace Mwabukusi
amesema misingi ya utawala bora katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu ni
muhimu ikazingatiwa ili Taifa liendelee kubaki moja kabla na baada ya uchaguzi
Mkuu
Amesema kuwa Watanzania wanahitaji haki na thamani ya kura yao kwa kuchagua viongozi wanaowataka na sio vinginevyo
"Wakati mwingine TLS imekuwa ikikemea na kuonesha wapi pa kurekebishwa na hili lisichukuliwe kama jambo baya bali ndo wajibu wetu na sisi hatuna maslahi binafsi" Amesisitiza Mhe.Mwabukusi
"Tunafanya hili kwa dhamira ya dhati ili kuhakikisha maslahi kwa umma ndo kipaumbele chetu.’’ Amesisitiza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wakati akiwasili kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka Mkuu wa Wanasheria unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa na baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wakiimba wimbo wa taifa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanasheria unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo.
Baadhi ya Wanachama wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wakiwa wamesimama wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiingia ukumbini kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Wanasheria unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Wanachama na Viongozi wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wanasheria unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo.
Baadhi ya Wanachama wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wakimsililiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Wanasheria unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wanachama na Viongozi wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) mara baada ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Wanasheria unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo.
No comments:
Post a Comment