Na. Mwandishi Wetu-Dar es Salaam
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene ametoa wito kwa Watanzania kumuenzi aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati
Mzee Cleopa David Msuya kwa kuendelea kudumisha umoja, amani na mshikamano na
kuyaenzi mazuri yote aliyoyafanya
enzi za uhai wake.
Mhe. Simbachawene
ameyasema hayo leo tarehe 22 Mei, 2025 alipoitembelea familia ya Hayati Msuya
nyumbani Upanga jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Simbachawene amesema Hayati Mzee Msuya atakumbukwa kwa kuwagusa watu wengi kwa namna
alivyokuwa na
upendo, kuwasaidia watu wengi pamoja
na kuhamasisha maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, Mhe. Simbachawene amemshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwathamini Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu kwa mujibu wa Sheria.
Akiongea kwa niaba ya familia, mtoto wa Hayati Msuya, Bi. Joyce Msuya-Mpanju
ameishukuru Serikali kwa mchango
wake mkubwa na
ushirikiano uliotolewa kwa familia hiyo tangu enzi za uhai wa Baba yao alipoanza kuugua hadi umauti
ulipomkuta na
kusimama bega kwa bega wakati wa msiba mpaka kukamlisha salama taratibu za
mazishi yake.
“Tunaishukuru
sana Serikali kwa kuwa pamoja na familia yetu tangu Mama
alipofariki mmekuwa na Baba bega kwa bega, hii ilisaidia sana hata kumfanya Baba
aishi maisha marefu maana tunaelewa mtu anapofiwa na Mwenza hali inavyokuwa. Mhe.
Waziri tunaomba utufikishie salamu zetu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samila Suluhu Hassan, Viongozi wote wa Serikali na Ofisi
unayoiongoza kwa upendo mliotuonesha kwetu,” Bi. Joyce ameongeza.
Hayati Cleopa Msuya alifariki dunia tarehe 7 Mei, 2025 na kuzikwa nyumbani kwake Kijiji cha Chomvu, Usangi Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro tarehe13 Mei, 2025.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Familia ya Makamu
wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati
Mzee Cleopa David Msuya (hawapo
pichani) alipoitembelea nyumbani kwao Upanga Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo kwa Familia ya Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Hayati Mzee Cleopa David Msuya (hawapo pichani) alipoitembelea
nyumbani kwao Upanga
Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI,
Bw. Xavier Daudi akifafanua jambo kwa Familia ya Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Hayati Mzee Cleopa David Msuya (hawapo pichani) wakati
Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. George Simbachawene (wa kwanza kulia) alipoitembelea
Familia hiyo nyumbani kwao Upanga
Jijini Dar es Salaam.
Mtoto wa Hayati
Mzee Cleopa David Msuya, Bi. Joyce Msuya Mpanju (aliyenyanyua mikono) akitoa
shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipoitembelea
Familia hiyo nyumbani kwao Upanga Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Utawala na Dawati
la Viongozi wa Kitaifa Wastaafu, Bi. Nyasinde Mukono akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (wa pili kutoka kulia) wakati Waziri
huyo alipoitembelea Familia ya Hayati Mzee Cleopa David Msuya nyumbani kwao Upanga
Jijini Dar es Salaam. Watatu kutoka kulia ni Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi na Wa kwanza kutoka kushoto ni
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi. Mary Mwakapenda.
Mtoto wa Hayati Mzee Cleopa David Msuya, Bw. Job Msuya
(katikati) akizungumza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipoitembelea
Familia hiyo nyumbani kwao Upanga Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja
na Familia ya Hayati Mzee
Cleopa David Msuya wakati alipoitembelea nyumbani kwao Upanga
Jijini Dar es Salaam. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa
Ofisi ya Rais-UTUMISHI.







No comments:
Post a Comment