Monday, November 30, 2015

WIKI YA UADILIFU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS

 


Simu ya Upepo "UTUMISHI", DSM.                               Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
Simu: 2118531/4 au 2122908                                      Utumishi House,
Barua Pepe:permsec@estabs.go.tz                                8 Barabara ya Kivukoni,
                                                                                       11404 Dar es Salaam.

                                                            30/11/2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 WIKI YA UADILIFU

Ofisi ya Rais –Menejimenti ya Utumishi wa Umma imenza Wiki ya Uadilifu katika Utumishi wa Umma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu leo ameongoza zoezi la kutoa Ahadi za Uadilifu kwa viongozi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Bw. Mkwizu alisema zoezi hilo ni endelevu na muhimu sana kwa Watumishi wa Umma hapa nchini.

“Tuishi viapo vyetu tulivyoahidi leo” Bw. Mkwizu alisisitiza na kusema ahadi hiyo iwe sehemu ya kazi ambapo inahusisha  ujazaji wa fomu ya Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma (PL.4), ambayo mhusika husaini kwa cheo alichonacho na Mtendaji Mkuu wa Taasisi yake.

Pamoja na masuala mengine, fomu hiyo itatumika pia kwa Watumishi wapya katika Utumishi wa Umma, mtumishi akibadilishwa cheo au kuhama ofisi.

Moja ya malengo ya fomu hiyo ni kuendeleza dhana ya Uwajibikaji, Usikivu kwa Umma na kuzingatia weledi katika Utumishi wa Umma. Fomu ya Ahadi ya Uadilifu inapatikana katika Tovuti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma yenye anuani, www.utumishi.go.tz.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kny: KATIBU MKUU - UTUMISHI



No comments:

Post a Comment