Wednesday, November 25, 2015

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kupunguza gharama za utekelezaji wa majukumu kwa watendaji na watumishi wa Umma nchini.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais , Utumishi Bw. Florence Temba (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa Serikali kutumia TEHAMA katika kufanya mikutano kwa njia ya Video (video conference) ambayo inapunguza gharama za uendeshaji wa vikao kazi serikalini. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi Kawawa. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Utumishi Bw. Florence Temba (katikati) akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani)faida za kutumia TEHAMA katika kuendesha vikao kazi serikalini. Kushoto ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Utumishi Bw. Florence Temba (kulia) akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu faida za matumizi ya TEHAMA katika kuendesha vikao kazi serikalini.Kushoto ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi Kawawa (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kati ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es asalam.Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba na Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kuhusu matumizi ya TEHAMA kupunguza gharama za mikutano kwa Taasisi za Serikali. 

No comments:

Post a Comment