Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA, Bw. Toshio Nagase (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (katikati) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari kwa Ofisi ya Rais -Utumishi katika ukumbi wa JICA mapema leo. Wa kwanza kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Mahusiano kwa Umma wa JICA, Bw. Raymond Msoffe. |
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ugavi na Ununuzi wa Ofisi ya Rais–Utumishi, Bw. Peter Mabale akihakiki vibali vya mojawapo ya gari lililokabidhiwa kwa Ofisi ya Rais - Utumishi kutoka JICA. |
Wawakilishi kutoka Ofisi ya Rais- Utumishi na JICA mara baada ya hafla ya makabidhiano ya magari katika ofisi za JICA jijini Dar es salaam. |
Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA Bw. Toshio Nagase (kushoto) akiangalia usajili wa mojawapo ya gari akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba mapema leo. |
Mojawapo ya gari lililokabidhiwa leo kwa Katibu Mkuu - Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. |
No comments:
Post a Comment