Monday, May 4, 2026

AFYA NI MTAJI – KATIBU MKUU MKOMI AWASISITIZA WATUMISHI WA UMMA KUJILINDA

Na. Antonia Mbwambo-Dodoma

Tarehe 04 Mei, 2026

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi amewasisitiza watumishi wa umma kulinda na kuimarisha afya zao wakati wote ili zitumike kuwajibika ipasavyo na kuwa mtaji katika kuleta matokeo chanya Serikalini.

Bw. Mkomi ameyasema hayo leo Mei 4, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba Jijini Dodoma wakati akihitimisha mafunzo kuhusu fursa za mimea tiba katika kutibu magonjwa mbalimbali. 

“Ni vizuri kila mtumishi wa umma akawa na uelewa kuhusu faida za utunzaji wa afya aliyo nayo na kuchukua hatua mapema pindi anapopata changamoto ili kuitumia afya hiyo kuwa mtaji Serikalini na kuleta tija katika maslahi ya umma”. Bw. Mkomi alisema.

Amesisitiza kuwa changamoto ya watumishi wengi kuugua mara kwa mara inapunguza kasi ya utendaji, lakini watumishi wanapokuwa na afya bora, hupunguza kuomba likizo za ugonjwa, na hivyo kuongeza bidii ya kazi.

Aidha, Bw. Mkomi amemshukuru Prof. Joseph Ndunguru ambaye ni Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA) kwa wasilisho lake ambalo limetoa uelewa kwa watumishi utakaojenga hamasa na kuwa nyenzo muhimu ya kuongeza ufanisi katika kazi.

Awali akiwasilisha mada kuhusu fursa za Mimea Tiba katika Kutibu Magonjwa mbalimbali, Prof. Ndunguru alisema Tanzania ina utajiri mkubwa wa mimea yenye uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali lakini bado inahitaji utafiti wa kisayansi ili kuthibitisha usalama na ufanisi wake.

Aliongeza kuwa matumizi ya tiba asili yaliyofanyiwa tafiti za kisayansi yanapunguza magonjwa, hivyo kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu na kuboresha afya ya watumishi. 

Prof. Ndunguru ametoa wito kwa Serikali na Taasisi za Umma kuwekeza katika tafiti ili kuendeleza tiba asili na kuchangia maendeleo ya afya na uchumi wa Taifa.

Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi akizungumza na watumishi wa Ofisi yake wakati alipokuwa akihitimisha mada ya mafunzo ya uelewa kwa ajili ya kuwajengea watumishi hao uwezo wa kiutendaji katika eneo maalumu la Ofisi hiyo lililopo Mtumba Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA) Prof. Ndunguru kwa wasilisho ambalo limetoa uelewa kwa watumishi utakaojenga hamasa na kuwa nyenzo muhimu ya kuongeza ufanisi katika kazi.

Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA) Prof. Ndunguru (kulia) akionesha vitabu ambavyo vinaelezea mikakati juu ya uhifadhi wa Mimea Tiba baada ya katibu Mkuu huyo kuhitimisha mafunzo ya uelewa  Mtumba jijini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi

Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wasaidizi Ofisi hiyo baada ya Katibu Mkuu huyo kuhitimisha mafunzo ya uelewa ya kila jumatatu yaliyofanyika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma.kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA)

Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi hiyo baada ya mafunzo ya uelewa ya kila jumatatu yaliyofanyika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma.Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru

Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi hiyo baada ya mafunzo ya uelewa ya kila jumatatu yaliyofanyika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma.Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru

Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mafunzo kuwajengea uwezo wa kiutendaji yaliyotolewa tarehe 4 Mei, 2026 na Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru (hayupo pichani ) katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma 

Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA) Prof. Ndunguru akitoa mafunzo kuhusu fursa za mimea tiba katika kutibu magonjwa mbalimbali kwa watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaliyofanyika Mei 4, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma.

Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mafunzo kuwajengea uwezo wa kiutendaji yaliyotolewa tarehe 4 Mei, 2026 na Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru (hayupo pichani ) katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma 


Viongozi na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mafunzo kuwajengea uwezo wa kiutendaji yaliyotolewa tarehe 4 Mei, 2026 na Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru (hayupo pichani ) katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma 




Katibu Mkuu-UTUMISHI (kushoto) Bw. Juma Mkomi (kushoto) akipokea pongezi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA) Prof. Ndunguru kwa kumkaribisha Mkurugenzi huyo kutoa Mafunzo ya uelewa katika Ofisi yake Mtumba Jijini Dodoma



No comments:

Post a Comment