Na. Antonia Mbwambo-Arusha
Tarehe 12 Mei, 2026.
Watumishi
wa Umma nchini wamehakikishiwa kuboreshewa mazingira ya kazi kadri uchumi
utakavyoruhusu ili kuleta tija katika utendaji kazi kwa maslahi ya umma.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika leo
tarehe 12 Mei, 2026 katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Mhe. Qwaray amesema, Serikali inatambua na
kuthamini mchango wa Watumishi wa Umma wote nchini wakiwemo Wauguzi, hivyo itazingatia
changamoto wanazokutana nazo watumishi hao, pamoja na kushughulikia kwa uzito
unaostahili ili kutengeneza mazingira mazuri ya
utendaji kazi.
"Niwahakikishie Serikali
itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na maslahi ya Watumishi wa Umma kadri
uchumi utakavyoruhusu kwani tunatambua mchango wenu mkubwa katika kuwahudumia Watanzania,
fanyeni kazi, Serikali ipo nanyi."
Mhe.
Qwaray alisema.
Aidha
Mhe. Qwaray ameongeza kuwa, ili kuwa na
ufanisi mkubwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi Serikali itaendelea
kuisimamia sekta ya afya pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma bila
kuathiri misingi ya Utumishi wa Umma, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa
ikiwemo uzingatiaji wa maadili.
Aidha amewataka kuwa na kauli
nzuri, huruma na upendo utakaoongeza tija
katika utendaji kazi ili kuleta mabadiliko chanya katika Sekta ya afya.
"Ninyi ndiyo watu wa kwanza kukutana
na mgonjwa pindi anapofika hospitali na ni watu wa mwisho mgonjwa anapotoka
hospitali baada ya matibabu, ikiwa mtakuwa na
nyuso za ukatili na ulimi mkali au wa kebehi, mtawakwaza wagonjwa na hata kuwakatisha
tamaa jambo ambalo litaonyesha mapungufu katika sekta ya afya.”Mhe. Qwaray
alisema.
Vilevile, Mhe. Qwaray amewaahidi Wauguzi hao kuwa
Ofisi imepokea masuala yote waliyoyaeleza katika risala yao na kuwaahidi kuyawasilisha kwa ajili ya kufanyiwa kazi ikiwemo
masuala ya Muundo Mpya wa Utumishi wa Kada ya Uuguzi na
Ukunga na Muundo wa Utawala katika
Sekta ya Afya ili kuboresha huduma ya afya na maslahi ya watumishi wa afya nchini.
Katika hatua nyingine, Naibu
Waziri Qwaray, ametoa wito kwa wauguzi kuhahakisha wanabadili mienendo na tabia
zisizopendeza wala kuendana na maadili ya kazi yao, lakini pia amewapongeza kwa
jitihada kubwa wanazozifanya katika kuwahudumia wananchi na kuboresha afya zao.
Kwa upande wake
Rais
wa Chama cha Wauguzi (TANNA), Dkt.
Ezekiel Mbao
amemshukuru Naibu Waziri, Mhe. Regina Qwaray kwa kujumuika nao kwenye
maadhimisho ya siku hiyo adhimu.
Maadhimisho hayo ya Siku ya Wauguzi Duniani yamebeba kauli mbiu isemayo Wauguzi Wetu, Mustakabali Wetu, Wauguzi Waliowezeshwa Huokoa Maisha.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray akizungumza
na Wauguzi kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania (hawapo pichani) wakati Naibu
Waziri huyo alipokuwa katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani
tarehe 12 Mei, 2026 katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray (aliyekaa katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Maadhimisho ya kilele
cha Siku ya Wauguzi Duniani mara tu baada ya Naibu waziri huyo kuhitimisha
Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika kuanzia tarehe 9 hadi 12, Mei, 2026 jijini
Arusha
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray, akitembelea
mabanda ya maonesho ya Wauguzi kujionea baadhi ya shughuli wanazozifanya katika
kuwahudumia Watanzania kabla ya Naibu Waziri huyo kuhitimisha Maadhimisho ya
Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika tarehe 12 Mei, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
Washiriki wa maadhimisho ya
Siku ya Wauguzi Dunuani wakifuatilia hotuba ya Mheni Rasmi ambaye ni Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati walipokuwa katika kilele cha Maadhimisho
ya Siku ya Wauguzi Duniani Jijini Arusha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray,akikabidhiwa
zawadi ya Chama cha Wauguzi (TANNA) na Raisi wa chama hicho Dkt. Ezekiel Mbao mara baada ya Naibu Waziri huyo kuhitimisha Maadhimisho
ya Siku ya Wauguzi Duniani tarehe 12 Mei, 2026 katika ukumbi wa AICC Jijini
Arusha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray, akisaini
kitabu cha wageni,mara tu baada ya kuwasili katika ukumbi wa AICC Arusha kwenye
Maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wauguzi Duniani
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray,akisalimiana
na baadhi ya viongozi wa chama cha wauguzi (TANNA) mara baada ya kuwasili
katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi
Duniani tarehe 12 Mei,2026.
Washiriki wa maadhimisho ya
Siku ya Wauguzi Dunuani wakifuatilia hotuba ya Mheni Rasmi ambaye ni Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati walipokuwa katika kilele cha Maadhimisho
ya Siku ya Wauguzi Duniani Jijini Arusha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray akikabidhi
zawadi kwa aliyekuwa Raisi wa chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) katika
Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani Jijini Arusha kama ishara ya kutambua
mchango alioutoa Raisi huyo wakati alipokuwa kiongozi wa Chama hicho katika kuhakikisha
wananchi wanapata huduma bora.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray,akipokea maelezo kuhusu shughuli mbalimbali wanazozifanya Wauguzi katika kuwahudumia wananchi, mara baada ya Naibu Waziri huyo kutembelea mabanda ya maonesho katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray akiwasili
katika ukumbi wa AICC Arusha tayari kwa kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya
Wauguzi Duniani yaliyofanyika kuanzia tarehe 9 hadi 12, Mei, 2026
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray,akifurahia
jambo wakati alipokuwa akifuatilia Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi
Duniani,yaliyofanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.






No comments:
Post a Comment