Sunday, May 31, 2026

RIDHIWANI: SERIKALI YALIPA ZAIDI YA BILIONI 24 MADAI YA WATUMISHI AONYA WATUMISHI WANAOGHUSHI BARUA ZA UHAMISHO, ASEMA 6 MBARONI KESI UHUJUMU UCHUMI

Na. Jawadu Kinyobwa


Serikali imeendelea kuboresha ustawi wa watumishi wa umma kwa kulipa malimbikizo ya mishahara yenye thamani ya Tsh. Bilipni 24,699,256,645.7 na kulipa watumishi 1,249 waliokoma utumishi yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 5,548,386,177.90.


Hayo yamebainishwa Juni Mosi, 2026 Mabele Hall jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) katika ufunguzi wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara na Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mtaa.


Pamoja na maboresho hayo, Mhe. Ridhiwani amesema  wapo baadhi ya waajiri ambao hawatekelezi ipasavyo wajibu wao katika kushughulikia madai ya aina hiyo ambapo hadi kufikia Mei 28,2026 madai ya watumishi 18,021 yenye jumla ya Shilingi 50,917,523,216 hayajawasilishwa Ofisini kwake.


“Baadhi ya waajiri wamekuwa wakiwasilisha katika Ofisi hii madai yenye kasoro ambazo walipaswa kuzibaini kabla hawajayawasilishwa.  Vile vile, yapo madai ya malimbikizo ya mshahara yanayotokana na waajiri kutozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika uendeshaji wa mashauri ya kinidhamu na hivyo kuzalisha madeni makubwa kwa Serikali” amesema.


Katika hatua nyingine, Mhe. Ridhiwani ametoa onyo kali kwa waajiri na viongozi wa taasisi za umma wanaokiuka sheria na taratibu za kiutumishi hususani kwa Waajiri kuchagua aina ya watu wa kufanya nao kazi, kutopokea watumishi wanaohamishiwa kwenye Taasisi zao, Waajiri kujimilikisha Taasisi na kuficha barua zenye maelekezo mahsusi ikiwemo barua za uhamisho.


Sambamba hayo, amesema Ofisi yake kwa kushirikiana na Taasisi za Haki Jinai imeanza kuchukua hatua mbalimbali kwa watumishi wanaojihusisha na ukiukwaji wa maadili ikiwemo kughushi barua za Ofisi hiyo ambapo hadi sasa jumla ya watuhumiwa Sita wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya Uhujumu Uchumi na kesi zinaendelea.


Awali akizungumza Katibu Mkuu Ofisi hiyo Juma Mkomi, amesema kikao hicho kimeandaliwa mahsusi kwa lengo la kutathmini nafasi ya wasimamizi wa Utawala na Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma, kubadilishana uzoefu katika kuboresha ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali hususan katika Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma hasa tunapoelekea kwenye utekelezaji wa Dira Mpya ya Taifa ya 2050.


Pia, Mkomi  amesema kikao hicho kitajikita  zaidi katika kujadili masuala muhimu ya Usimamizi wa Utumishi wa Umma, Usimamizi  na matumizi ya Mifumo ya TEHAMA Serikalini, changamoto zilizopo katika utekelezaji wa majukumu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na namna bora ya kukabiliana nazo.


Kikao kazi hicho kina kauli mbiu isemayo “Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Sikivu, Jumuishi, Wenye Matokeo na Uwajibikaji kuelekea Dira 2050”.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akizungumza   na Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu  (hawapo pichani) katika ufunguzi wa kikao kazi kilichofanyika Juni 1, 2026 katika ukumbi wa Mabele Hall jijini Dodoma. 


Katibu Mkuu,Ofisi ya Raia-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi, akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara na Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mtaa kilichofanyika Juni 1, Jijini Dodoma.



Sehemu ya Viongozi na Watendaji kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete wakati alipokuwa akizungumza nao katika  wa ufunguzi wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Jijini Dodoma 


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akitoa utambulisho wa viongozi na washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kabla ya ufunguzi wa kikao hicho Juni 1, 2026 Jijini Dodoma


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete (kulia ) akiteta jambo na Katibu Mkuu-UTUMISHI  Bw. Juma Mkomi (kushoto) wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara na Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mtaa kilichofanyika Juni 1, Jijini Dodoma. 



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi hiyo mara baada ya Waziri huyo kufungua 
kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Jijini Dodoma

Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete wakati akizungumza nao katika ufunguzi wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Jijini Dodoma

Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (kulia) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Jijini Dodoma


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akizungumza   na Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu  (hawapo pichani) katika ufunguzi wa kikao kazi kilichofanyika Juni 1, 2026 katika ukumbi wa Mabele Hall jijini Dodoma. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete (mwenye suti ya kijivu ) akifurahia jambo na viongozi wengine kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, mara baada ya Wazuri huyo kufungua kikao kazi kilichofanyika Juni 1, 2026 katika ukumbi wa Mabele Hall jijini Dodoma. 

No comments:

Post a Comment