Tuesday, April 14, 2026

WATUMISHI WA UMMA WASISITIZWA KULINDA AFYA

 Na: Eric Amani, Mtumba Dodoma

 13 Aprili, 2026

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Juma Mkomi ametoa rai kwa kila mtumishi wa umma kuhakikisha analinda afya ya mwili na akili kuanzia nyumbani kwa kuwa mtumishi mwenye afya njema anakuwa na uwezo wa kufikiri na kufanya uamuzi sahihi katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Juma Mkomi wakati akiongoza kikao cha kuchagua mfanyakazi bora wa Ofisi yake kilichofanyika Aprili 13, 202katika ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma.

Bw. Mkomi aliongeza kuwa, watumishi wanapaswa kujenga utamaduni wa kujali afya zao kwa kuzingatia lishe bora, kufanya mazoezi ya mwili pamoja na kupata muda wa kupumzika ambapo masuala yote hayo huanzia katika mazingira ya nyumbani.

Watumishi wa umma wanapokuwa na afya dhaifu, utendaji kazi hushuka na hivyo kuathiri moja kwa moja utendaji kazi mahala pa kazi. Hivyo amewakumbusha watumishi hao kuwa afya njema ni msingi imara katika utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi.

Aidha, Katibu Mkuu huyo ametumia fursa ya kikao hicho kuitakia kila la kheri Utumishi Sports Club ambayo inaelekea kwenye mashindano ya Mei Mosi yatakayofanyika mkoani Njombe.

Bw. Mkomi amewahimiza wachezaji pamoja na benchi la ufundi kujituma, kudumisha nidhamu na kuzingatia maadili ya michezo ili kuiwakilisha vyema ofisi.

Nendeni kwenye mashindano hayo muhimu na onesheni nidhamu njema na kiwango bora zaidi cha ushindani ukilinganisha na kiwango mlichoonesha wakati wa mashindano ya SHIMIWI 2025 Zingatieni nidhamu, mshikamano na ushirikiano ili kuendelea kuleta ushindi katika ofisi yetu” alisisitiza Bw. Mkomi.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw, Juma Mkomi akizungumza na maofisa wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa kikao cha kuchagua Mfanyakazi bora katika Ofisi yake April 13, 2026 katika viwanja vya ofisi hiyo iliyopo Mtumba, Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais – UTUMISHI Bw. Mussa Magufuli akifungua Kikao cha kuchagua mfanyakazi bora kilichofanyika April 13, 2026 katika Viwanja vya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi w Umma na Utawala Bora katika Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi na Wakurugenzi wasaidizi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Mwenyekiti (Hayupo Pichani)  wa Kikao cha Kuchagua Mfanyakazi Bora wakati anazungumza na watumishi wa ofisi hiyo kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza April 13, 2026 Mtumba Jijini Dodoma.


Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (Aliyesimama) wakati wa akitoa neno kwenye kikao cha kuchagua Mfanyakazi Bora wa ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma April 13, 2026.


Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakipiga Kura kwa ajili ya kuchagua mfanyakazi bora katika kikao cha kuchagua Mfanyakazi Bora wa mwaka 2026 kwenye viwanja vya ofisi hiyo Aprili 13, 2026 Mtumba, Jijini Dodoma.

Picha ya Pamoja ya washiriki wa kinyang’anyiro cha Mfanyakazi Bora katika Ofisi ya Rais – UTUMISHI kutokea Kurugenzi na Idara mbalimbali zilizopo ofisi hiyo wakati wakisubiria kumchagua mfanyakazi bora wa ofisi Mtumba, Jijini Dodoma April 13, 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi Akimkabidhi Zawadi aliyekuwa Mtumishi wa Ofisi hiyo Bi. Maria Felix baada ya Kumaliza Muda wake wa Utumishi wa Umma katika Ofisi hiyo April 13, 2026 Mtumba, Jijini Dodoma.


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi akipokea na kuzindua jezi mpya kutoka kwa nahodha wa timu ya mpira wa pete Bi. Elizabeth Fussi Aprili 13, 2026 katika viwanja vya ofisi hiyo kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mkoani Njombe kwa ajili ya mashindano ya Mei Mosi.


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi akipokea na kuzindua jezi mpya kutoka kwa nahodha wa timu ya mpira wa miguu Bw. Cyprian Lasway Aprili 13, 2026 katika viwanja vya ofisi hiyo kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mkoani Njombe kwa ajili ya mashindano ya Mei Mosi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi  akimpongeza Bi. Gladness Mwanri kutokea Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma kwa kuchaguliwa kuwa Mfanyakazi Bora 2026 wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Aprili 13, 2026 Jijini Dodoma. 



Sehemu ya wachezaji wa timu ya mpira wa pete wakiwa katika viwanja vya ofisi ya Rais – UTUMISHI wakati wa uzinduzi wa jezi yao mpya wanaotarajia kuivaa katika mashindano ya Mei Mosi yanayofanyika Mkoani Njombe. 



No comments:

Post a Comment