Wednesday, April 22, 2026

NAIBU KATIBU MKUU,OFISI YA RAIS-UTUMISHI BW. XAVIER DAUDI AKUTANA NA VIONGOZI WA JICA KWA MAZUNGUMZO

 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi akutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma. Viongozi hao wamemtambulisha Mwakilishi Mkuu Mpya Bw.Kuge Katsuya baada ya Bw.Ara Hitoshi kumaliza muda wake.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi (aliyevaa suti ya bluu) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) baada ya viongozi hao kuhitimisha mazungumzo yaliyofanyika Aprili 22, 2026 katika Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mwakilishi Mkuu Mpya Bw.Kuge Katsuya na kushoto kwake ni Mwakilishi Mkuu aliyemaliza mda wake Bw.Ara Hitoshi



Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi (kulia) akipokea baadhi ya nyaraka kutoka kwa Mwakilishi Mkuu Mpya Bw.Kuge Katsuya (kushoto) baada ya viongozi hao kuhitimisha mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi (wa pili kutoka kulia) akifurahia jambo baada ya kuhitimisha mazungumzo baina ya Ofisi yake na JICA Mtumba Jijini Dodoma.



No comments:

Post a Comment