Na. Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe
21 Aprili, 2026
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Felister Shuli amewasisitiza Watumishi wa Umma kushughulikia kwa haki na kwa wakati mrejesho unaowasilishwa na wananchi kupitia Mfumo wa (e- Mrejesho) ili kujenga imani na heshima ya Serikali kwa umma.
Bi. Shuli ameyasema hayo leo
Aprili 21, 2026 wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi katika
ufunguzi wa mafunzo ya matumizi ya kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko,
mapendekezo, maulizo na pongezi kwa watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Taasisi
zilizo chini yake.
“Ili kufikia utumishi wa umma unaowajibika
na uliotukuka, ni vizuri tukashughulikia mrejesho wa wananchi kwa haki na
uharaka zaidi.” Bi Shuli alisema.
Amesema, Watumishi wa Umma
wanapaswa kuwa na mabadiliko katika fikra, mitazamo, mifumo na tabia walizonazo
ili kuwa na Utumishi wa Umma wenye matokeo chanya na thamani halisi kwa mwananchi.
Bi Shuli ameongeza kuwa uzingatiaji
wa maadili katika utumishi wa umma si kuzifuata tu Sheria, Kanuni, Taratibu na
Miongozo ya Utumishi wa Umma bali ni pamoja na kuutumia ipasavyo utaalamu unaohusu
ushughulikiaji wa mrejesho wa wananchi .
Amesema ni jukumu la kila
mshiriki kuonesha ushirikiano na kuzingatia utu hususani wanapotoa huduma kwa
wateja pamoja na kuwa waaminifu hasa katika utunzaji siri kwa kuwa kazi
watakazofanya zitahitaji kuwa na matumizi sahihi ya taarifa.
Aidha, amewapongeza washiriki
wote kwa kuhudhuria mafunzo hayo na kuwataka wajifunze kwa bidii ili wawe
wataalamu watakaowajibika kikamilifu
Kwa upande wake mwenyekiti wa
kikao hicho ambaye ni Afisa TEHAMA kutoka Watumishi Housing Investiments (WHI) Bw.
Albano Lukiano amemshukuru Bi. Shuli kwa
kuwafungulia mafunzo hayo na kuahidi kuwa yale yote watakayofundishwa watayazingatia
na kuyafanyia kazi ili kutoa huduma bora kwa manufaa ya umma.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Felister (kushoto)
akiteta jambo na Mwenyekiti wa mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa e-Mrejesho
ambaye pia ni Afisa TEHAMA kutoka Watumishi Housing Investiments (WHI) Bw.
Albano Lukiano (kulia) kabla ya Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo hayo jijini
Dodoma.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Felister Shuli (aliyekaa
katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya matumizi ya kutuma, kupokea
na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi kwa watumishi mara
baada ya Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa
Ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Felister Shuli
(kushoto) akifurahia jambo mara baada
ya Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo ya kutumia Mfumo wa e-Mrejesho
yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za
Taifa Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Maadili wa Ofisi hiyo Bi. Janet Mishinga
Afisa
tawala kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Bi. Semeni Muyabhaga akiwasilisha mada ya wakati wa mafunzo ya matumizi
ya Mfumo wa e-Mrejesho yaliyofanyika Aprili 21, 2026 katika ukumbi wa
Ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa kikao cha mafunzo ya kutumia Mfumo wa e-Mrejesho Bw. Albano Lukiano akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Felister Shuli mara baada ya Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Jijini Dodoma.
Afisa
Rasilimaliwatu Mwandamizi Kutoka Idara ya Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Hassan Kilenza akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa mjadala
wa hoja mbalimbali kuhusu matumizi ya Mfumo wa e-Mrejesho jijini Dodoma.
Washiriki
wa mafunzo ya matumizi ya kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko,
mapendekezo, maulizo na pongezi kwa watumishi wakifuatilia hotuba ya mgeni
Rasmi wakati alipokuwa akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika leo Aprili 21, 2026
jijini Dodoma.
Washiriki
wa mafunzo ya matumizi ya kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko,
mapendekezo, maulizo na pongezi kwa watumishi wakifuatilia hotuba ya mgeni
Rasmi wakati alipokuwa akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika leo Aprili 21, 2026
jijini Dodoma.
Washiriki
wa mafunzo ya matumizi ya kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko,
mapendekezo, maulizo na pongezi kwa watumishi wakifuatilia hotuba ya mgeni
Rasmi wakati alipokuwa akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika leo Aprili 21, 2026
jijini Dodoma.
Afisa Tawala kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Stella Teri akiwasilisha mada kuhusu uzingatiaji wa Kanuni za Maadili ya Utendeji kwa watumishi wa Umma wakati wa mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa e-Mrejesho yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Jijini Dodoma
Afisa
rasilimali watu mwaandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Bi. Saada Ibrahim akiwasilisha mada ya wakati wa mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa e-Mrejesho yaliyofanyika Aprili 21, 2026 katika ukumbi wa Ofisi
ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Jijini Dodoma.

No comments:
Post a Comment