Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa,
Mhe. Abdallah Chaurembo akipongeza utendaji kazi wa Mamlaka ya Serikali mtandao
(eGA) mara baada ya kamati yake kupatiwa mafunzo kuhusu usalama wa serikali mtandao
yaliyolenga kutoa elimu hiyo kwa wajumbe wa kamati hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusiana na masuala ya serikali Mtandao, mara baada ya eGA kutoa mafunzo ya usalama wa serikali mtandao kwa wajumbe wa kamati hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe akichangia hoja kuhusu
serikali mtandao, mara baada ya kupatiwa mafunzo ya usalama wa serikali mtandao
yaliyotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ambaye
pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Kusini Unguja (CCM) Mhe. Mwantumu Dau Haji
akichangia hoja kuhusu serikali mtandao, mara baada ya kupatiwa mafunzo ya
usalama wa serikali mtandao yaliyotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA),
Mhandisi Benedict Ndomba akitoa ufafanuzi wa hoja za masuala ya serikali
mtandao zilizowasiloishwa wa wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, mara baada ya kamati hiyo
kupatiwa mafunzo kuhusu usalama wa serikali mtandao.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA),
Mhandisi Benedict Ndomba akiwasilisha mada ya usalama wa serikali mtandao kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, mara
baada ya kamati hiyo kupatiwa mafunzo kuhusu usalama wa serikali mtandao.
No comments:
Post a Comment