Tuesday, September 6, 2022

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA MAJENGO MENGINE YA WIZARA YANAYOJENGWA KATIKA AWAMU YA PILI YA UJENZI WA MJI WA SERIKALI



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na watendaji wa wizara mbalimbali mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa ofisi za wizara unaotekelezwa katika awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. 

 

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Waziri Mkuu iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za wizara unaotekelezwa katika awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Sehemu ya watendaji wa wizara mbalimbali wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati akihitimisha ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa ofisi za wizara unaotekelezwa katika awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. 

 

 

Mhe. Jenista Mhagama na Mhe. Joyce Ndalichako pamoja na Mhe. Deogratius Ndejembi wakijadiliana jambo kabla ya kumpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa ofisi za wizara unaotekelezwa katika awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwasalimiana na watendaji wa wizara mbalimbali waliojitokeza kumsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati akihitimisha ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa ofisi za wizara unaotekelezwa katika awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. 

 

Mwonekano wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora linaloendelea kujengwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

 

No comments:

Post a Comment