Na. James K. Mwanamyoto-Magu
Tarehe 23 Februari, 2023
Mhe.
Jenista ametoa wito huo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo
ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa Zahanati ya Kijiji cha Ihayabuyaga, Halmashauri
ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza inayojengwa na TASAF kupitia ufadhili wa Umoja wa Nchi zinazosambaza Mafuta Duniani (OPEC).
Mhe.
Jenista amewasisitiza wananchi kuwa mstari wa mbele katika usimamizi wa miradi
mbalimbali ya maendeleo ambayo ikikamilika kwa wakati inawanufaisha kwa
kuwapatia huduma bora kama ilivyokusudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe.
Jenista amesema, Serikali imekusudia kila fedha ya mradi inayotolewa, itumike
vizuri na ndio maana kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) imeanzisha programu maalum ya TAKUKURU RAFIKI aliyoizindua Disemba
20, 2022 jijini Dodoma ikilenga kuwashirikisha wananchi na wadau katika kuzuia
vitendo vya rushwa nchini.
“Kupitia TAKUKURU RAFIKI, wananchi wanakuwa ni
sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya TAKUKURU katika mapambano dhidi ya vitendo
vya rushwa, hivyo tutoe taarifa ya viashiria au uwepo wa vitendo vya rushwa
bila woga kwani TAKUKURU RAFIKI ipo kwa ajili hiyo,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Mhe.
Jenista ameongeza kuwa, hivi sasa TAKUKURU RAFIKI ipo karibu na kila Mtanzania
kwa lengo la kuhakikisha kila mradi unatekelezwa vizuri, hivyo ni wajibu wa
kila mwananchi kuitumia fursa ya TAKUKURU RAFIKI kulinda fedha za umma zinazotokana
na kodi ambazo zinachangiwa na wananchi.
Kwa
upande wake, Mbunge wa Jimbo la Magu mkoani Mwanza, Mhe. Boniventura Kiswaga
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kujenga nyumba ya watumishi katika Zahanati ya Kijiji cha
Ihayabuyaga kupitia fedha za TASAF ili kutatua changamoto ya wananchi kuchelewa
kupatiwa huduma kutokana na watumishi wa zahanati hiyo kuishi mbali na kituo
cha kazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Mwanza iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya TASAF.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akitoa maelekezo ya ukamilishwaji wa miundombinu katika nyumba
ya watumishi wa Zahanati ya Kijiji cha Ihayabuyaga, Halmashauri ya Wilaya ya
Magu, mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza
uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo
ya TASAF wilayani humo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista
Mhagama akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi
wa Kijiji cha Ihayabuyaga, Halmashauri ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza (hawapo
pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa
watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya TASAF
wilayani humo.
Sehemu
ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Kijiji cha
Ihayabuyaga, Halmashauri ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa
miradi ya maendeleo ya TASAF wilayani humo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akisalimiana na viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Magu mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya kikazi iliyolenga
kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo
ya TASAF wilayani humo.
Mbunge
wa Jimbo la Magu mkoani Mwanza, Mhe. Boniventura Kiswaga akitoa salamu za
shukrani kwa Serikali kujenga nyumba ya watumishi katika Zahanati ya Kijiji cha
Ihayabuyaga kupitia fedha za TASAF ili kutatua changamoto ya wananchi kuchelewa
kupatiwa huduma kutokana na watumishi wa zahanati hiyo kuishi mbali na kituo
cha kazi.
Mwonekano wa nyumba ya watumishi wa Kituo cha Afya, inayojengwa
kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Kijiji cha Ihayabuyaga,
Halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment