Tarehe 21 Februari, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amewaelekeza viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Nyamagana mkoani Mwanza kusimamia ukamilishaji wa miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ya afya na elimu ili itoe michango katika maendeleo ya taifa.
Mhe.
Jenista ametoa maelekezo hayo kwa nyakati tofauti katika Wilaya ya Ilemela na
Nyamagana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya
TASAF mkoani Mwanza.
Mhe.
Jenista amesema hukuna sababu ya kusuasua katika ukamilishaji wa miradi hiyo ya
afya na elimu kwa kuwa ni miradi muhimu sana na ikizingatiwa kuwa fedha yote ya
ujenzi wa miradi hiyo ilishatengwa na kutolewa na Serikali ya Awamu ya Sita.
Mhe.
Jenista amesisitiza usimamizi mzuri wa miradi hiyo ya afya na elimu ambayo Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia TASAF
ametoa fedha nyingi ili iwanufaishe walengwa na kuboresha utoaji wa huduma
katika sekta hizo muhimu kwa jamii.
Mhe.
Jenista amesema miradi yote ya elimu inayotekelezwa na TASAF itasaidia sana
kuandaa rasilimaliwatu itakayoendeleza kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya
Awamu ya Sita ya kuleta maendeleo chanya kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
“Shule
hizi zinazojengwa kama zitatoa elimu bora kwa wanafunzi na wakapata ufaulu
mzuri, nina hakika watakuwa ndio madaktari, walimu, wahandisi, wabunge, wakuu
wa wilaya na viongozi wa vyama vya siasa wajao na kuongeza kuwa TASAF inandaa
rasilimaliwatu ya kesho itakayokuwa na tija kwa maendeleo ya taifa,” Mhe.
Jenista amesisitiza.
Akizungumzia
faida ya miradi ya afya inayotekelezwa na TASAF, Mhe. Jenista amesema miradi
hiyo ikikamilika itatoa huduma bora za afya kwa watumishi wa umma na wananchi
ili waweze kuwa na afya bora inayowawezesha kushiriki shughuli mbalimbali za
kiuchumi na kijamii zitakazowawezesha kutoa mchango katika maendeleo ya taifa.
“Tukiwa
na afya njema, tutashiriki vizuri shughuli mbalimbali za kiuchumi na hatimaye
utekelezaji wa miradi ya afya ya TASAF utakuwa umechangia katika maendeleo ya
taifa letu,” Mhe. Jenista amefafanua.
Kwa
upande wake, mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyamagana, Bi. Rachel
Juma amesema, wanafunzi wa shule hiyo wanaahidi kutomuangusha Rais wa Awamu ya
Sita Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusoma kwa bidii ili kuunga mkono
jitihada zake za kuboresha mazingira ya shule yao kupitia fedha za TASAF.
Mwanafunzi
mwingine wa shule hiyo ya Nyamagana, Bi. Zeana Deus amesema kuwa, atayatumia
vema madarasa yaliyojengwa na TASAF ili kutimiza ndoto yake ya kufanya vizuri katika
masomo ya sayansi kwa ajili ya maisha yake ya baadae na kutoa mchango katika
maendeleo ya taifa.
Naye
Bw. Shaban Jafari ambaye pia ni mwanafunzi wa shule hiyo ya Sekondari Nyamagana
amesema kuwa, awali kabla ya TASAF kujenga madarasa katika shule yao walikuwa
wakikabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa, hivyo wanamshukuru Rais wa
Awamu ya Sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwajengea madarasa kupitia TASAF.
Sanjari
na hao, Mkazi na Mlengwa wa TASAF wa Wilaya ya Nyamagana Bi. Ratifa Zanziba
ameishukuru TASAF kwa kujenga madarasa na mabweni katika Shule ya Sekondari ya
Nyamagana ambapo imewaondolea adha wanafunzi kulazimika kwenda umbali mrefu
kuitafuta elimu.
Mkazi
mwingine ambaye pia ni mlengwa wa TASAF Wilaya ya Nyamagana Bi. Ziada Basil
ameungana na mwenzie kuishukuru TASAF kwa kujenga madarasa na zahanati katika
wilaya yao ili kuwahudumia wananchi wa eneo hilo.
TASAF
imeendelea kugusa maisha ya wananchi katika Wilaya ya Ilemela na Nyamagana mkoani
Mwanza kupitia utekelezaji wa miradi yake ya Afya na Elimu ambayo inafadhiliwa
na Umoja wa Nchi zinazosambaza Mafuta Duniani (OPEC).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza
na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Mtaa wa Jiwe Kuu
na Mihama, Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wakati wa
ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani Ilemela
mkoani Mwanza.
Sehemu ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na
Wananchi wa Mtaa wa Jiwe Kuu na Mihama, Kata ya Kitangiri,
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista
Mhagama alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara
yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.
Adam Malima wakifurahia jambo walipokuwa wakisikiliza
taarifa ya utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilaya ya Ilemela wakati wa ziara ya
kikazi ya Mhe. Jenista ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.
Adam Malima wakifurahia jambo walipokuwa wakisikiliza
taarifa ya utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilaya ya Ilemela wakati wa ziara ya
kikazi ya Mhe. Jenista ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza
na viongozi na watumishi wa Mkoa wa Mwanza alipowasili mkoani humo kwa ziara ya
kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Nyamagana pamoja na Wananchi wa Kata ya Butimba wakati wa
ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF inayofadhiliwa
na Umoja wa Nchi zinazosambaza Mafuta Duniani (OPEC) katika Halmashauri ya
Manispaa ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyamagana
na wananchi wa Kata ya Butimba wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa
akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi
ya TASAF inayofadhiliwa na Umoja wa Nchi zinazosambaza Mafuta Duniani (OPEC) katika
Halmashauri ya Manispaa ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Mwonekano wa jengo la bweni la wanafunzi wa shule ya
Sekondari Nyamagana linalojengwa na Serikali kupitia TASAF chini ya ufadhili wa
Umoja wa Nchi zinazosambaza Mafuta Duniani (OPEC) katika Halmashauri ya
Manispaa ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwasisitiza viongozi
na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Nyamagana juu ya ukamilishaji wa
ujenzi mabweni ya Shule ya Sekondari Nyamagana wakati wa ziara yake ya kikazi
ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF inayofadhiliwa na Umoja wa Nchi
zinazosambaza Mafuta Duniani (OPEC) katika Halmashauri ya Manispaa ya Nyamagana
mkoani Mwanza.
Mmoja wa
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyamagana, Zeana Deus akiishukuru Serikali
kupitia TASAF kwa kujenga madarasa na mabweni shuleni hapo yatakayowasaidia
kupata elimu bora ili watimize malengo yao.
No comments:
Post a Comment