Na. Veronica E. Mwafisi-Njombe
Tarehe 23 Februari, 2023
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewaasa watumishi wa umma nchini kuwahudumia vizuri wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zitolewazo na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Ndejembi wito huo kwa watumishi wa umma, wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Mji Njombe mkoani Njombe kilicholenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao katika halmashauri hiyo.
Mhe. Ndejembi amesema, kila mtumishi wa umma nchini akitimiza wajibu wake kuna uwezekano mkubwa wa kutatua matatizo ya wananchi kwani kila mtumishi wa umma kwa nafasi yake ni mwakilishi wa Serikali hivyo anapaswa kuilinda taswira ya Serikali kwa kutoa huduma nzuri kwa wananchi ili wananchi wajivunie uwepo wa serikali yao.
Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, watumishi wa umma wanapaswa kutoa huduma bora kwa wananchi kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesimamia na anaendelea kusimamia vema masilahi ya watumishi wote wa umma nchini, hivyo ni wajibu wa kila mtumishi kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni sehemu ya kuthamini na kuunga mkono jitihada hizo za Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe, Mhe. Erasto Mpete amemshukuru Naibu Waziri Ndejembi kwa kufanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Mji Njombe ili kuhimiza uwajibikaji, kusikiliza na kutatua kero za watumishi wa halmashauri hiyo kitendo ambacho kimejenga ari na morali ya utendaji kazi wa watumishi wa umma katika halmashauri yake.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi anaendelea
na ziara yake ya kikazi katika
Halmashauri ya Mji Njombe kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa
umma, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na
kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Halmashauri hiyo ya mji
mkoani Njombe.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza
na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Mji Njombe, wakati wa ziara yake ya
kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi
hao na kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF katika Halmshauri hiyo
ya mji mkoani Njombe.
Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Mji
Njombe wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipokuwa akizungumza nao wakati
wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi hao na kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF katika Halmshauri
hiyo mkoani Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Kissa
Gwakisa akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma na kukagua
utekelezaji wa Miradi ya TASAF katika wilaya yake wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu
Waziri huyo katika Halmshauri ya Mji Njombe mkoani Njombe.
Mkuu wa Idara ya Utawala na
Utumishi, Halmashauri ya Mji Njombe, Bi. Ester Zullu akisoma taarifa ya
utumishi ya halmashauri hiyo ya mji kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji,
kutatua changamoto zinazowakabili watumishi na kukagua
utekelezaji wa Miradi ya TASAF katika Halmshauri hiyo ya mji.
Mtumishi wa Halmashauri ya Mji Njombe, Dkt. Stephano Mbapila akiwasilisha hoja ya kiutumishi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF katika Halmshauri hiyo ya mji mkoani Njombe.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akisikiliza
hoja iliyokuwa ikiwasilishwa na mtumishi wa Halmashauri ya Mji Njombe wakati wa
ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF katika Halmshauri hiyo
ya mji mkoani Njombe.
No comments:
Post a Comment