Na. Veronica Mwafisi-Makete
Tarehe 21 Februari, 2023
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka
walengwa wa TASAF Wilayani Makete kuchangia nguvu kazi yao ya asilimia 10 ili
kuwezesha ukamilishaji wa miradi ya TASAF ya ujenzi wa miundombinu kwa wakati katika
Shule ya Sekondari Mang’oto ambayo inatekelezwa kwa ufadhili wa Umoja wa
Nchi zinazosambaza Mafuta Duniani (OPEC).
Mhe. Ndejembi ametoa wito huo kwa
walengwa wa TASAF, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya mradi
wa ujenzi wa bwalo la chakula katika shule ya Sekondari Mang’oto iliyopo katika
Kijiji cha Mang’oto, Halmashauri ya Wilaya ya Makete, mkoani Njombe.
“Wananchi wa Mang’oto nawaomba mjitoe kutekeleza
miradi mbalimbali ya miundombinu inayowataka kuchangia nguvukazi yenu ya
asilimia 10 ili mshiriki kukamilisha miradi hiyo kwa wakati,” Mhe. Ndejembi
amesisitiza.
Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya
jitihada za kutafuta fedha kwa wadau wa maendeleo kuiwezesha TASAF kutekeleza
miradi yake kwa lengo la kujenga miundombinu yenye tija kwa maendeleo ya taifa.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Makete, Mhe.
Festo Sanga, amemhakikishia Mhe. Naibu Waziri Ndejembi kuwa, atawahamasisha
wananchi wa jimbo lake wachangie nguvu kazi ili kuwezesha miradi yote ya TASAF
inayotekelezwa katika jimbo lake ikamilike kwa wakati.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa
Shule ya Sekondari Mang’oto, Bw. Prince Mwenda amesema, wanaishukuru Serikali
ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaboreshea
mazingira ya kupata elimu kupitia ujenzi wa mabweni, madarasa, bwalo na nyumba
za walimu.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi anaendelea na ziara ya kikazi ya wiki moja mkoani Njombe
kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF pamoja na kuhimiza
uwajibikaji kwa watumishi wa umma mkoani huo.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi na wanafunzi wa Kijiji cha Mang’oto
mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa bwalo la chakula katika Shule ya
Sekondari Mang’oto linalojengwa kwa ufadhili wa TASAF, wakati wa ziara ya
kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika
Halmashauri ya Wilaya Makete mkoani Njombe.
Baadhi
ya wananchi na wanafunzi wa Kijiji cha Mang’oto wakimsikiliza Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi wakati akizungumza nao mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa bwalo
la chakula katika Shule ya Sekondari Mang’oto linalojengwa kwa ufadhili wa
TASAF, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya Makete mkoani
Njombe.
Mbunge wa Makete, Mhe. Festo Sanga
akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya
kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika
Halmashauri ya Wilaya Makete mkoani Njombe.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi na wanafunzi wa Kijiji cha Mang’oto
mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa bwalo la chakula katika Shule ya
Sekondari Mang’oto linalojengwa kwa ufadhili wa TASAF, wakati wa ziara ya
kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika
Halmashauri ya Wilaya Makete.
Mwonekano bwalo
la chakula katika Shule ya Sekondari Mang’oto linalojengwa na Serikali kupitia TASAF
katika Halmashauri ya Wilaya Makete mkoani Njombe.
No comments:
Post a Comment