Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na
watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili (hawapo pichani) wakati wa kikao
kazi chake na watumishi wa Idara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa
Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya
Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara hiyo.
Sehemu
ya watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na
watumishi hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba
jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara yao na kuhimiza
uwajibikaji kwa watumishi wa Idara hiyo. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa
Idara hiyo, Bi. Leila Mavika.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akipokea Mwongozo wa
Mavazi kwa watumishi wa umma toka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa
Maadili, Bi. Leila Mavika mara baada ya Naibu Waziri huyo kuhitimisha kikao
kazi chake na watumishi wa Idara hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo
na kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Ukuzaji wa
Maadili, Bw. Ally Ngowo akiwasilisha taarifa kwa Naibu waziri, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ya utekelezaji
wa majukumu ya sehemu anayoisimamia (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha
Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili kilichofanyika
katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la
kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.
No comments:
Post a Comment