Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma
Tarehe 12 Machi, 2023
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba
na Sheria, Mhe. Florent Kyombo amesema kamati yake imejipanga kikamilifu kutekeleza
wajibu wa kuisimamia, kuishauri na kuipa mwongozo sahihi Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake ili ziweze
kutoa mchango wenye tija katika maendeleo ya taifa na kufikia lengo la kutoa
huduma bora kwa wananchi.
Mhe. Kyombo
amesema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha kamati yake na viongozi pamoja
na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kilicholenga kuwasilisha muundo na majukumu
ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi
zake kwa kamati hiyo.
Mhe. Kyombo amesisitiza kuwa, wajumbe wa kamati yake wako tayari
kufanya kazi ya kuishauri ipasavyo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora na taasisi zake ili kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muuungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuujenga Utumishi wa Umma
unaowajibika kwa wananchi.
Aidha, Mhe. Kyombo ametoa wito kwa watendaji wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake, kila mmoja kwa
nafasi yake kutimiza wajibu wake ili kuiwezesha kamati yake kutekeleza jukumu
la kushauri na kusimamia vema utendaji kazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake.
Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema watendaji wa
ofisi yake wanategemea sana mwongozo wa Mwenyekiti na wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawalaz, Katiba na Sheria utakaowawezesha kutekeza majukumu
yao kikamilifu ili kufikia lengo la kuboresha utoaji huduma bora kwa wananchi
kama ilivyokusudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Utawala Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo akiongoza kikao
kazi cha kamati yake na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kilicholenga
kuiwezesha kamati hiyo kupokea wasilisho la muundo na majukumu ya Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake.
Mhe. Yahaya Massare (aliyeinua mkono) akiwasilisha
hoja wakati wa kikao kazi cha Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na viongozi pamoja na
watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, kilicholenga kuiwezesha kamati hiyo kupokea wasilisho
la muundo na majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora na taasisi zake.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa ufafanuzi wa
muundo na majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati
wa kikao kazi cha kamati hiyo na watendaji wa ofisi yake.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria, Mhe. Abdullah Mwinyi akiwasilisha hoja wakati wa kikao
kazi cha Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na viongozi pamoja na
watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, kilicholenga kuiwezesha kamati hiyo kupokea wasilisho
la muundo na majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora na taasisi zake.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria, Mhe. Ahmed Ngwali akiwasilisha hoja wakati wa kikao
kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba
na Sheria na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kilicholenga
kuiwezesha kamati hiyo kupokea wasilisho la muundo na majukumu ya Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria, Mhe. Suleiman Zedi akiwasilisha hoja wakati wa kikao
kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba
na Sheria na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kilicholenga
kuiwezesha kamati hiyo kupokea wasilisho la muundo na majukumu ya Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akiwaongoza watendaji wa
taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI kujibu hoja za wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao
kazi cha kamati hiyo na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora na taasisi zake.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete na Naibu Katibu Mkuu wa
ofisi yake Bw. Xavier Daudi wakipokea hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala Katiba na Sheria wakati wa kikao
kazi cha kamati hiyo na watendaji wa ofisi yake.
No comments:
Post a Comment