Na. James K. Mwanamyoto-Dar es Salaam
Tarehe 28 Machi, 2023
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amekitaka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) na Taasisi ya UONGOZI kuandaa programu za mafunzo zitakazowajengea uwezo kiutendaji watumishi wa umma na viongozi ili watoe huduma bora kwa wananchi na mchango katika maendeleo ya taifa.
Mhe. Kikwete ametoa maelekezo hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Chuo cha Utumishi wa Umma na Taasisi ya UONGOZI iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hizo.
Mhe. Kikwete amesema, watumishi wa umma na viongozi walio katika taasisi zote za umma wanahitaji kupata mafunzo yenye tija kwa ajili ya kukuza taaluma zao na kuongeza ufanisi kiutendaji, hivyo ni jukumu la Chuo cha Utumishi wa Umma na Taasisi ya UONGOZI kuhakikisha watumishi na viongozi wanapata mafunzo yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Mhe. Kikwete amesisitiza kuwa, Chuo cha Utumishi wa Umma kinatoa mafunzo kwa watumishi ambao wameshaajiriwa na Serikali, hivyo wanahitaji kuandaliwa programu nzuri za mafunzo zitakazoimarisha utendaji kazi wao.
Sanjari na hilo, Mhe. Kikwete amekipongeza Chuo cha Utumishi wa Umma kwa kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma wanaokaribia kustaafu ili kuwaandaa wawe na maisha mazuri baada ya kustaafu kuutumikia umma.
“Binafsi naamini Chuo cha Utumishi wa Umma mnafanya jambo zuri kuwapatia mafunzo watumishi wanaokaribia kustaafu kwa mujibu wa sheria, hivyo mkijipanga vizuri nina uhakika hawataharibikiwa pindi wakistaafu,” Mhe. Kikwete amesisitiza.
Akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya UONGOZI, Mhe. Kikwete ameusisitiza uongozi wa taasisi hiyo kubuni programu za mafunzo ambazo zitawaandaa viongozi wa baadae, kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekusudia.
Mhe. Kikwete ameongeza kuwa, Rais wa Awamu ya Sita, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatamani kuona Taasisi ya UONGOZI inatoa mchango wa kuwaandaa viongozi watakaoendeleza kazi nzuri iliyofanywa na uongozi wake.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amehitimisha siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi jijini Dar es Salaam ya kuzitembelea taasisi zilizo chini ya ofisi yake ili kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Menejimenti ya Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji wa watumishi wa taasisi hiyo.
Sehemu ya Menejimenti ya Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji wa watumishi wa chuo hicho.
Kaimu Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Ernest Mabonesho akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwasili katika Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma chuo hicho.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Menejimenti ya Chuo cha Utumishi wa Umma mara baada ya kuwasili chuoni hapo jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma chuo hicho.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya UONGOZI jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji wa watumishi wa taasisi hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika kikao kazi na Menejimenti ya Taasisi ya UONGOZI jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji wa watumishi wa taasisi hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika kikao kazi na Menejimenti ya Taasisi ya UONGOZI jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji wa watumishi wa taasisi hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji wa watumishi wa taasisi hiyo kwa watumishi wa Taasisi ya UONGOZI jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment